HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 15, 2020

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KATIKA KUJIAJIRI

 Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kagera, Halima Bulembo, akizungumza na vijana katika kongamano hilo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, Sera na Watu wenye Ulemavu,  Anthony Mavunde, akizungumza katika kongamano hilo.
 Sehemu ya vijana hao wakizungumzia changamoto zinazowakabili.


Na Lydia Lugakila, Kagera


Vijana Mkoani Kagera wametakiwa kuondokana na  kutegemea ajira toka Serikalini badala yake wajijengee mazingira ya kuwezeshwa kwa kukaa katika makundi ili wanufaike na fursa mbalimbali zitolewazo na serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, Sera na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, katika Kongamano la Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Kagera chini ya Mwenyekiti wa UVCCM, Happiness Runyogote.

Akizungumza na vijana hao wakiwemo wenye ulemavu, Anthony Mavunde, amesema anatambua moja ya changamoto ya ukosefu wa kipato na ajira na kuwa si kila mmoja anaweza kuajiriwa katika sekta rasmi bali vijana wanapaswa kuondokana na utegemezi wa ajira badala yake wajitengenezee makundi yatakayowawezesha kupata fulsa mbali mbali kwa uraisi.

Amesema vijana wengi wanaamini kuwa
ajira ni kukaa maofisini wakati wapo vijana waliofanikiwa kupitia kilimo, uvuvi hata kujiajiri katika biashara ya kuuza matunda na kupata mafanikio.

Waziri Mavunde amesema serikali inathamini vijana na tayari imeweka mipango kabambe ya kuwasaidia vijana ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa makundi katika jamii, wenye ujuzi, wasio wajuzi, walioishia darasa la saba, wenye ulemavu, wenye vipaji na katika hatua ya elimu, kujikusanya katika mfumo wa vikundi ili waweze kunufaika na fursa mbali mbali.

"Ajira sio ofisini vijana nawahimizeni tengeneza mazingira ya kuwezeshwa fursa haina mataili kuwa ikufuate ulipo badala ya kuilaumu serikali kaeni katika makundi fulsa zitawakuta katika makundi" alisema Naibu waziri huyo.

Amesema vijana lazima wafanye biashara halali na yenye kuwaingizia kipato ili wakipewa nguvu wawe na kianzio.

Aidha amesema wananchi wenye uwezo wa kufanya kazi hapa nchini kuanzia miaka 15 ni Milioni 24.3 huku akieleza kuwa ifikapo mwaka 2021 vijana Milioni 4.4 watahitajika.

Kwa upande wake  Mbunge wa Viti Maalum mkoani Kagera, Halima Bulembo, amesema atahakikisha anatoa ushirikiano kwa vijana huku akiwahimiza kutokuchagua kazi.

Joanifaith Kataraia ni mjumbe kamati ya utekelezaji taifa amewasihi vijana kufanya kazi na kubadilika na kuyafanyia kazi maelekezo yanayotolewa na serikali ili kunufaika na kuachana na kulilia ajira.

Hata hivyo vijana walionufaika na kongamano hilo ni kutoka wilaya za Karagwe, Misenyi, Muleba, Ngara, Biharamulo, Wilaya ya Bukoba mjini, Halmashauri ya wilaya ya Bukoba.

No comments:

Post a Comment

Pages