Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, akiandika maelezo yanayotolewa na Kamishna Msaidizi Omar Khamis Omar (kulia),
wakati alipotembelea Shule ya Polisi Moshi Tanzania, mwishoni mwa wiki kufuatilia masuala mbalimbali katika shule hiyo inayofundisha fani tofauti
zenye lengo la kuzuia na kupambana na uhalifu nchini. Kushoto ni Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Tunu Ng’ondya.
Kamishna Msaidizi Omar Khamis Omar, akisoma taarifa ya
maendeleo ya mafunzo mbalimbali yanayoendelea katika Shule ya Polisi Moshi
Tanzania kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
wakati naibu waziri alipotembelea shule hiyo, mwishoni mwa wiki kufuatilia masuala mbalimbali katika shule hiyo inayofundisha fani tofauti
zenye lengo la kuzuia na kupambana na uhalifu nchini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Salum
Hamduni akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia) na Uongozi wa Shule ya Polisi Moshi Tanzania,mwishoni
mwa wiki ikiwa ni ziara yenye lengo la kufuatilia masuala mbalimbali katika shule hiyo inayofundisha fani tofauti
zenye lengo la kuzuia na kupambana na uhalifu nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni akizungumza na Kamishna Msaidizi Omar Khamis Omar (kulia) na Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Tunu Ng’ondya wakati
alipotembelea Shule ya Polisi Moshi Tanzania,mwishoni mwa wiki kufuatilia
masuala mbalimbali katika shule hiyo inayofundisha fani tofauti zenye lengo la
kuzuia na kupambana na uhalifu nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment