Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifungua sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB
Benki ya CRDB imefanya hafla ya kusherehekea ‘Siku ya Wanawake Dunia’ ikilenga kuhamasisha usawa wa kijinsia katika jamii. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya CRDB inachukulia kwa umuhimu suala la kumuwezesha mwanamke na ndiomana
Benki hiyo imetoa kipaumbele cha ajira kwa wanawake katika ngazi mbalimbali. “Asilimia 46 ya wafanyakazi wetu ni wanawake, na tunatamani kuona tunaongeza
kufikia asilimia 50,” alisema Nsekela.
Benki ya CRDB imefanya hafla ya kusherehekea ‘Siku ya Wanawake Dunia’ ikilenga kuhamasisha usawa wa kijinsia katika jamii. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya CRDB inachukulia kwa umuhimu suala la kumuwezesha mwanamke na ndiomana
Benki hiyo imetoa kipaumbele cha ajira kwa wanawake katika ngazi mbalimbali. “Asilimia 46 ya wafanyakazi wetu ni wanawake, na tunatamani kuona tunaongeza
kufikia asilimia 50,” alisema Nsekela.
Nsekela alisema Benki ya CRDB pia inafanya jitihada za kuwanyanyua wanawake kupitia nafasi za uongozi huku akibainisha kuwa Benki hiyo ina jumla ya wanawake viongozi 284 katika ngazi za umeneja, wakuu wa vitengo na wakurugenzi. Nsekela alisema Benki ya CRDB imedhamiria kujenga mazingira, rahisishi, mazuri na rafiki ya kujenga usawa ili kuwasidia wanawake waweze kukua katika mazingira yao ya kazi.
Katika hafla hiyo Benki ya CRDB pia ilizindua kampeni maalum ya kusaidia kutoa taulo za kike (sanitary pads) kwa wanafunzi mashuleni. Kampeni hiyo ilianza kwa kuzindua zoezi la uchangiaji lilokuwa likiendeshwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa ambapo wafanyakazi wa Benki ya CRDB wamejitokeza kuchangia gharama za ununuzi wa taulo hizo. “Tunashukuru Mkurugenzi wetu Mtendaji ametufungulia kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1, hii ni zawadi ya kipekee kwa wanawake wote lakini pia inaonyesha ni kwa namna
gani anawathamini wake,” alisema Mwambapa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully
Mwambapa akiendesha zoezi la uchangiaji kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa taulo za kike (sanitary pads) kwa wanafunzi mashuleni.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully
Mwambapa na viongozi wengine wanawake wakishangilia baada ya Mkurugenzi
Mtendaji, Abdulmajid Nsekela kuchangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia
wanafunzi wakike
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Benki ya CRDB, Siophoro Kishimbo
alisema Benki hiyo imeweka mikakati endelevu ya kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanawake
wa Benki hiyo wanapata fursa sawa na wanaume. “Tunaihamasisha jamii kuzingatia
usawa katika sehemu zote iwe ni kwenye kazi na hata nyumbani kwenye familia hii
itaongeza ushiriki wa wanawake katika shughuli za maendeleo na hivyo kujenga
taifa imara zaidi,” alisema Kishimbo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela (wakwanza kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara, Dkt. Joseph Witts, Mkurugezi
wa Rasilimali Watu, Siophoro Kishimbo na Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick
Nshekanabo, wakionyesha vibao vyenye ujumbe wa kuhamasisha usawa wa kijinsia katika
jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela
akiwatambulisha baadhi ya viongozi wanawake wa Benki hiyo, kutoka kulia ni
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Tully Esther Mwamba, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa
Wateja, Yolanda Uriyo na Mkuu wa Kitengo cha Mikikati ya Bishara, Jessica
Nyachiro.
Salamu kuelekea
maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, 2020
Meneja wa Tawi la Benki ya CRDB Kariakoo, Diana
Mtalo akielezea safari yake katika uongozi kama mwanamke na kuwahamasisha
wanawake wengine kujiamini na kufanya kazi kwa bidi katika maeneo yao ya kazi.
Mwandishi wa Habari wa Channel 10 faraja
Kihongole alikuwa miongoni mwa washiriki wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment