HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 13, 2020

BODI YA USHIRIKA KCU YATAKIWA KULIPA DENI LA MILIONI 12 KWA WAKULIMA WA KAHAWA-KAGERA

Na Alodia Dominick, Bukoba

Vyama vya Ushirika vya KDCU Ltd na KCU 1990 Ltd vilivyopo mkoani Kagera vimetakiwa kutenga Sh. 30 kutoka katika ushuru wa vyama vya msingi (Amcos) kwa ajili ya kumkopesha mkulima wa kahawa.

Akizungumza  na wakulima wa zao la kahawa mkoani hapa Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema ili mkulima wa kahawa aendelee kupenda ushirika lazima uwepo mfuko wa kutunza fedha ambao utamsaidia katika kipindi kigumu ambacho anataka kupeleka watoto shule na matatizo mengine ya kifamilia aweze kukopa katika mfuko huo.

Bashe ameongeza kwamba wakulima wa zao la kahawa wamekuwa wakiuza kahawa changa ikiwa bado shambani (Obutura) kwa bei ndogo na kuwauzia maseneta si kwa kupenda ni kwa sababu wanakuwa na hali ngumu ya kifedha na hivyo wanaamua kuuza kahawa hiyo, dawa ni kuwepo mfuko utakaowakopesha fedha ambazo zitakuwa hazina riba katika kipindi kigumu ili anapouza kahawa anarejesha fedha hiyo.

"Ushirika utaendelea kuwepo hauwezi kufa kitu cha msingi ni kubuni mbinu nzuri ambazo zitasaidia wakulima wetu kuacha kuuza kahawa kwa maseneta na badala yake kuendelea  kuuzia ushirika, na jambo hilo ni kuanzisha mfuko wa kuwakopesha wanachama bila riba".Alisema waziri Bashe.

Ameagiza bodi ya KCU Ltd kupitia kwa meneja wake kuanzisha mfuko huo kwa msimu 2020/2021 baada ya KDCU ltd kuwa tayari wameanzisha mfuko huo.

Meneja wa chama cha ushirika cha wilaya za Karagwe na Kyerwa KDCU ltd Osca Dominick amesema katika ushirika huo tayari wanao mfuko huo na kwa msimu 2019/2020 wamekusanya shilingi milioni 900.

Naye meneja wa chama kikuu cha ushirika KCU 1990 ltd Edson Rugeimukamu ameeleza kuwa kwa msimu 2020/2021 wataanzisha mfuko huo ili uweze kuwasaidia wakulima wao.

Mmoja wa wakulima hao, Kazungu Gordian kutoka wilaya ya Muleba amesema chama cha msingi alichomo walikuwa na wanachama zaidi ya 200 lakini kwa sasa wamebaki wanachama hai 10 kutokana na wanachama kutoona faida ya ushirika hivyo kutokana na mfuko huo ambao utakuwa unawakopesha wanachama huenda ushirika ukarudisha heshima yake ya miaka ya nyuma.

Hata hivyo Bashe ametoa siku tatu kwa bodi ya ushirika wa KCU 1990 Ltd kuwa wamelipa deni la wakulima waliouza kahawa yao katika ushirika huo kwa msimu 2019/2020 kiasi cha Sh. Milioni 12.

No comments:

Post a Comment

Pages