Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt.
Jasson Rweikiza (Mb), akizungumza na mnufaika wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini (TASAF), Bibi Edith Brayson Makala jana ambaye anafanya
shughuli za ushonaji wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la
kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt.
Jasson Rweikiza (Mb), akishuhudia moja na bidhaa iliyotengenezwa na
mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Bibi Edith Brayson
Makala wakati wa ziara ya kamati hiyo jana yenye lengo la kukagua
utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt.
Jasson Rweikiza (Mb), akizungumza na baadhi ya wanufaika wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mtaa wa Sokoine, Kata ya Misuna, Manispaa
ya Singida wakati wa ziara ya kamati hiyo jana yenye lengo la kukagua
utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.
Baadhi
ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mtaa wa
Sokoine, Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida wakimsikilza Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt.
Jasson Rweikiza (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao jana
wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa
miradi ya Serikali mkoani Singida.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akizungumza na baadhi ya
wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Mtaa wa Sokoine,
Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida (hawapo pichani) wakati wa ziara ya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa jana yenye
lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Bw. Ladislaus
Mwamanga akiwasalimia wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
(TASAF), Mtaa wa Sokoine, Kata ya Misuna, Manispaa ya Singida (hawapo
pichani) wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na
Serikali za Mitaa jana yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya
Serikali mkoani Singida.
James Mwanamyoto - Singida
Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Bibi Edith Brayson Makala mwenye umri wa miaka 55 mkazi wa Manispaa ya Singida, Mtaa wa Sokoine, amesimamia vema Kauli Mbiu ya HAPA KAZI TU ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli ambayo imemuwezesha kuinua uchumi wa familia yake kupitia ruzuku
ya TASAF.
Pombe Joseph Magufuli ambayo imemuwezesha kuinua uchumi wa familia yake kupitia ruzuku
ya TASAF.
Akitoa ushuhuda jana, mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida, Bibi Makala amesema, baada ya kufanya kazi za ajira ya muda chini ya Mpango wa TASAF, aliweza kununua cherehani mbili zanye thamani ya shilingi 400,000/= kupitia ujira wa kazi hizo ambazo anazitumia katika shughuli za ushonaji wa nguo ikiwemo sare mbalimbali za shule pamoja na mashuka.
“Nimelenga kushona sare za shule kwani ni biashara endelevu kwa kuwa watoto wanasoma kila siku na kila mwaka, hivyo ninaboresha maisha yangu na familia kwa ujumla kupitia shughuli hiyo” Bibi Makala amefafanua.
Aidha, Bibi Makala ameieleza Kamati hiyo ya Bunge kuwa, ametumia fedha za ruzuku alizopata
kulipa ada za watoto wake ambapo mmoja wao amefikia elimu ya chuo kikuu.
Bibi Makala ameelezea malengo yake ya baadae kuwa, ni kujikwamua kutoka kwenye umaskini na kuweza kuzisaidia kaya maskini zinazomzunguka.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb) amesema, kamati yake imeridhishwa na jitihada zinazofanywa na wanufaika wa TASAF akiwemo Bibi Makala baada ya kuwatembelea wanufaika hao na kujionea shughuli wanazozifanya.
Mhe. Dkt. Rweikiza ametoa rai kwa wanufaika wote nchini kutumia vema ruzuku wanayoipata ili kujikwamua kutoka katika umaskini, na kuongeza kuwa Kamati yake itaendelea kufanya ufuatiliaji wa namna fedha za Serikali zinavyotumiwa na wanufaika.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) amesema mara baada ya Mhe. Rais kuzindua Awamu ya Tatu, Sehemu ya Pili ya Mpango wa TASAF, Serikali imepanga kuzifikia kaya zote maskini
nchini.
Bibi Edith Brayson Makala, kabla ya kunufaika na Mpango alikuwa akiishi maisha magumu kwa
kutegemea biashara ya kuuza maji aliyokuwa akiifanya mume wake.
kutegemea biashara ya kuuza maji aliyokuwa akiifanya mume wake.
No comments:
Post a Comment