HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 13, 2020

Kifaransa chapigiwa chapuo Afrika Mashariki

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier akiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Liberat Mfumukeko wakati wa kusaini makubalino ya kusaidia masomo ya Kifaransa ili lugha hiyo itumike kwenye Jumuya hiyo.


Na Mwandishi Wetu, Arusha

BALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier, amesaini makubaliano ya kuwezesha masomo ya lugha ya Kifaransa ili iwe miongoni mwa lugha itakayotumika kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Hafla ya kusaini makubaliano hayo ilifanyika jijini Arusha kati ya Balozi Clavier na Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Liberat Mfumukeko.

Ziara ya balozi huyo wa Ufaransa imekuja siku chache kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya siku 12 za Maonesho ya tamaduni za Kifaransa yatakayohusisha nchi mbalimbali zinazozungumza kifaransa.

Maonesho hayo yatahudhuriwa na watu mbalimbali wanaozungumza na kuipenda lugha hiyo wakiongozwa na mabalozi 13 wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania ambao wanazungumza Kifaransa.

Nchi zinazozungumza kifaransa ambazo balozi zao zipo Tanzania ni Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Morocco, Switzerland, Misri, Canada, Visiwa vya Comoro, Burundi, Vihetnam, Ubelgiji, Rwanda, Senegal, Visiwa vya Shelisheli na Ufaransa yenyewe.

Maadhimisho ya 50 ya kuzungumza Kifaransa yataanza Machi 17 hadi 28 jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Allience Francie.

No comments:

Post a Comment

Pages