HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 30, 2020

JOKATE: VIONGOZI WA DINI TOENI ELIMU YA ULIPAJI KODI

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Afisa Ardhi Mteyule Wilaya ya Kisarawe, Jumanne Mwampashe (kati kati), na Mkuu wa Kitengo cha Kodi Kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami wakiteta jambo mara baada ya kikao na Uongozi wa Shule ya Mtakatifu  Dorcas iliyopo Kata ya Kazimzumbwe ambayo inamilikiwa na mtu binafsi na inadaiwa pango la kodi ya Ardhi takribani milioni 98, tangia mwaka 2009 hadi sasa.

Na Asha Mwakyonde, aliyekuwa Pwani

VIONGOZI wa dini wameshauriwa kutoa elimu ya ulipaji kodi pango ya ardhi kwa waumini wao kwani wengi hawana uelewa wa ulipaji wa kodi hiyo pamoja na umiliki wa ardhi.

Pia Shule ya Msingi Mtakatifu Dorcas Vigama iliyopo wilayani Kisarawe, Pwani inadaiwa kodi pango ya ardhi kiasi cha milioni 98 tangu  tangu mwaka 2009 hadi sasa na  shule ya sekondari ya Seminari inayomilikiwa Kanisa la KKKT Ushirika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambayo nayo inadaiwa milioni 239.

Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kama msimamizi wa shughuli za Serikali alipotembelea Taasisi zinazodaiwa kodi ya pango la ardhi Wilayani humo kwa lengo la kujua kwa nini hazijalipa kodi stahiki kwa Serikali.

Katika ziara yake Mkuu huyo wa Wilaya ya Kisarawe aliongozana na Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Denis Masami ambaye alisema kodi ya pango la ardhi ni moja ya sifa za umiliki ardhi.

Katika kikao na uongozi wa shule ya Mtakatifu Dorcas, Jokate amesema ifike mahali watu waache tamaa ya kumiliki maeneo makubwa ambayo wanashindwa kuyasimamia na kuyaendeleza.

Jokate amesisitiza, Taasisi ya Mtakatifu Dorcas  nayomiliki takribani ekari 77 ambazo siyo zote zimeendelezwa na hivyo kusababisha baadhi ya maeneo kuvamiwa.

Ameongeza kwamba mtu anaweza kupoteza sifa ya umiliki ardhi pale anapovunja masharti ya umiliki ikiwa ni pamoja na kutokulipa kodi ya pango la ardhi kwa mujibu wa sheria.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema wananchi wengi wanamaeneo lakini hawana hati za umiliki jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya nchi kwani  kwa kutokuwa na uelewa wa kulipa kodi stahiki.

" Hata nyie viongozi wa dini mnapokuwa kwenye ibada muwahamasishe na kutoa elimu kwa waumini wenu juu ya umuhimu wa ulipaji kodi ili waweze kulipa kodi," amesema mkuu huyo wa Wilaya.

Amesema  serikali ya awamu ya tano imefanya miradi mikubwa ikiwamo barabara, hospitali, vituo vya afya na kwamba huduma nyingi zimeboresha  ambazlo zinatokana na kodi mbalimbali zinazolipwa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Kodi  Wizara ya Ardhi ,Denis Masami amesema  kuwa wameridhishwa na juhudi za Mkuu wa wilaya hiyo na kwamba maelekezo yake wanayafanyia kazi.

"Tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wawe na uelewa mpana juu ya masuala ya ulipaji kodi pango ya ardhi, kulipa kodi kunakfanya ardhi yako kuwa miliki salama  na asiyelipa kodi anahatarisha umiliki wake," aliaema Masami.

Kwa upande wa shule ya Mtakatifu  Dorcas, mtunza fedha wa shule hiyo Reymond Lyimo alikiri kupokea hati ya madai ya kodi ya pango la ardhi na kwamba analikubali deni hilo kwa sababu hawana kumbukumbu yeyote inayoonesha deni hilo kulipwa.  Katika hali ya kujitetea kuhusu madai hayo ya kodi ya pango la ardhi,.

Uongozi wa shule ya Mtakatifu Dorcas ulidai kodi hiyo ilikuwa inalipwa na aliyekuwa msimamizi wa shule hiyo japo hakuna kumbukumbu zozote ofisini za kuthibitisha malipo hayo.

Hata hivyo Afisa Ardhi Mteule wa Wilaya ya Kisarawe Jumanne  Mwampashe amessema, Taasisi ya Mtakatifu Dorcas ilishawahi kulipa malipo ya awali tuu kwa maana ya malipo ya umilikishaji na hivyo deni la milioni 98 ambalo ni kodi ya pango la ardhi ni deni sahihi kwa vile hawana taarifa wala nyaraka zinazoonesha malipo zaidi ya yale ya umilikishaji.

Uamuzi wa kuzitembelea taasisi hizo umetokana na mkakati maalum wa Wizara ya ardhi wa kuwatambua wadaiwa wote wa kodi ya pango la ardhi na kuwatembelea ili kujua kama kuna changamoto zozote zinazowafanya wasilipe kodi ambayo ipo kwa mujibu wa sheria pamoja na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kulipa kodi husika.

No comments:

Post a Comment

Pages