HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 30, 2020

NMB YATOA SH. MILIONI 100 MAPAMBANO DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Kama mchango wa Benki ya NMB katika kudhibiti na kupambana dhidi ya virusi vya Corona, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB-Ruth Zaipuna amekabidhi msaada wa kifedha shilingi Milioni 100 kwa Mhe. Waziri Mkuu - Kassim Majaliwa mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Ummy Mwalimu pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali. Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi ya Waziri Mkuu-Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu - Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto) akipokea hundi ya Sh. Milioni 100 kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna (wa nne kutoka kushoto) Kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa Serikali wa NMB Alfred Shao na kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu- Kassim Majaliwa akizungumza na uongozi wa Benki ya NMB.  

Benki ya NMB ikiwa na maadhimio sawa ya kuudhibiti ugonjwa huu, mchango huu utaisaidia serikali katika mapambano dhidi ya virusi hivi.

Tunasisitizwa kuendelea kutumia njia stahiki kujikinga na maambukizi.

#TanzaniaBilaCoronaInawezekana
#JikingeMlindeMwenzio

No comments:

Post a Comment

Pages