Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa meli mpya, chelezo na Ukarabati wa Meli ya MV Victoria jijini Mwanza, Mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Eric Hamissi.
Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Kampuni ya KTMI ya Korea Kusini inayofanya ukarabati wa meli Meli ya MV Victoria jijini Mwanza, Mwishoni mwa wiki, wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wake.
Muonekano wa Chelezo inayojengwa katika bandari ya Mwanza South ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 96. Kukamilika kwa chelezo kutarahisisha matengenezo ya meli katika Ziwa Victoria.
Muonekano wa meli ya MV Victoria mara baada ya ukabati mkubwa ambao mpaka sasa umefikia asilimia zaidi ya 96. Meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mzigo wa tani 200.
No comments:
Post a Comment