Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic, akifafanua jambo kwa walimu na wanafunzi waliohudhulia hafla ya makabidhiano ya chumba cha darasa jipya ambacho kimejengwa kwa ajili ya kusomea watoto wa elimu ya awali katika shule ya msingi Kibwegere. (Picha na Victor Masangu).
NA VICTOR MASANGU, UBUNGO
SEKTA ya elimu hapa nchini licha ya serikali ya awamu ya
tano kuweka sera ya kutoa elimu bure
lakini bado katika baadhi ya maeneo ya shule za msingi na Sekondari zilizopo
katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam zinakabiliwa na changamoto mbali
mbali ya upungufu wa matundu ya vyoo pamoja na uhaba na uchakavu wa miundombinu ya madarasa hivyo kusababisha
wanafunzi wengine kusoma katika mlundikano mkubwa.
Katika kuliona hilo Shirika lisilokuwa la kiserikali la
Organization Community Development (OCODE) limeamua kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano
Dk. John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa msaada wa
madawati 39,ya wanafunzi, viti 13 vya kukalia walimu pamoja na kukabidhi rasmi
chumba cha darasa moja jipya kwa ajili
ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya msingi Kibwegere.
Akizungumzia kuhusiana na msaada huo Mkurugenzi wa Shirika
la Ocode Joseph Jackson amesema kwamba kwa sasa wana tekeleza mradi wa elimu
ambao utakuwa wa kipindi cha miaka
mitano ambao umeanza kufanyika tangu 2019- 2023 kwa lengo la kuwez kuwasaidia
watoto wa shule za awali na msingi katika kuwawekea mazingira mazuri katika
suala zima la upatikanaji wa kupata elimu iliyo bora kwa manufaa yao ya baadae.
Aidha Mkurugenzi huyo
alibainisha kwamba katika mradi huo umeweza kugusa ujenzi wa darasa hilo jipya
la wanafunzi wa elimu ya awali ambalo mpaka kukamilika kwake limegharimu kiasi
cha shilingi milioni 26 na kwamba wana imani kuwa watoto hao kwa sasa waliokuwa
wanakabiliwa na changamoto ya kukaa kwa mlindikano watasoma katika mazingira
ambayo ni rafiki kwao
“Shirika letu la Ocode kwa sasa linaendelendea kutekeleza program
ya mradi wa elimu ambao utakuwa unazigusa baadhi ya shule za msingi ambazo zipo
katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es salaam, maana nia yetu ni
kuwasaidia watoto hawa kuanzia elimu ya awali na kwamba kwa sasa tutajikita
zaidi kwa wanafunzi wa daras ala kwanza na darasa la pili pamoja na wale
wanafunzi wa ngazi ya awali ili kuweza kuwajengea uwezo wa kupata elimu bora,”alisema
Mkurugenzi huyo.
Pia alibainisha kwamba katika kipindi cha utekelezaji wa
mradi huo kwa kipindi cha miaka mitano watahakikishwa kwamba wanashirikiaa bega
kwa began a serikali ya awamu ya tano pamoja na wadau wengine wa maendeleo ili
kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia elimu kuanzia ngazi za chini na
kuendelea.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kibwegre akisoma risala kwa mgeni rasmi katika halfa ya
makabidhdiano ya madawati na uzinduzi wa darasa hilo amebainisha kwamba kwa sasa
wanafanya kazi katika mazingira magumu sana kutokna na ukosefu wa ofisi za
walimu na vyumba vya madarasa ambapo wakati mwingine inawalazimu walimu
kufanyia kazi zao wakiwa wamekaa chini ya miti hivyo msaada huo ambao umetolewa
na Ocode utakuwa ni mkombozi kwa upande wao.
“Shule yetu ya Kibwegere kwa kweli tunapenda kutoa shukrani
zetu za kipekee kwa Shirika ili la Ocode kwani wameweza kutuona na kutusaidia
katika mambo mbali mbali ya kutujengea
darasa moja, kutupa viti, pamoja na madawati ya wanafunzi hii kwa upande wetu ni
moja ya hatua, kwani hapo awali hali ilikuwa ni ngumu kutokana na miundombinu
yenyewe ya madarasa pamoja na ofisi za walimu, hivyo napenda kushukuru sana,”alisema
Kulemba.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice
Dominic ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya makabidhiano amesema kwamba
pamoja na juhuzi zinazofanywa na serikali lakini amekiri bado kunachanagmoto
kubwa ya miundombinu ya madarasa kwa shule ya msingi na sekondari na anatambua
walimu wanafanya kazi zao katika mazingira magumu sana hivyo amelipongeza
shirika la Ocode kwa kuamua kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya
elimu kuanzia ngazi ya awali.
SHULE ya msingi Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya Ubungo
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa
sasa ina jumla ya wanafunzi 1741 ambao wanakabiliwa na changamoto mbali mbali
ikiwemo upungufu wa walimu, uhaba wa miundombinu ya madarasa, ofisi za walimu,
pamoja na matundu ya vyoo.
No comments:
Post a Comment