Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea Mradi wa
Ujenzi wa Jengo la Kituo cha Polisi Mkokotoni, kilichopo Kaskazini Unguja, Zanzibar.Kamati
hiyo imefika kukagua mradi huo baada ya kituo cha awali kuungua katika ajali ya
moto iliyosababishwa na hitilafu za umeme.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mjumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ,Ulinzi na Usalama, Prosper Mbena, akikagua
ukuta wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la
Kituo cha Polisi Mkokotoni, kilichopo Kaskazini Unguja, Zanzibar.Kulia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. Kamati hiyo imefika
kukagua mradi huo baada ya kituo cha awali kuungua katika ajali ya moto
iliyosababishwa na hitilafu za umeme.
Na
Mwandishi Wetu
Katika kukidhi haja ya
Kituo cha Polisi baada ya kituo cha awali kuteketea kwa ajali ya moto, serikali
imewakikishia wananchi wa eneo la mkokotoni, Kaskazini Unguja kukamilika kwa
mradi huo ndani ya muda wa miezi mitatu
na kuweza kusaidia masuala ya ulinzi na usalama katika maeneo hayo
pamoja na maeneo ya kisiwa cha tumbatu ambacho hutegemea huduma ya ulinzi
kutoka katika kituo hicho.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea na kukagua
maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha polisi ambacho ni kituo cha daraja B.
“Katika kuhakikisha
tunaendelea kulinda raia na mali zao pamoja na changamoto za ofisi askari wetu
wameendelea kufanya kazi katika kituo cha awali na sisi serikali tunaendelea
kusimamia kituo hiki kiwe kimekamilika ndani ya miezi mitatu na kiujumla
tunaishukuru kamati ya bunge kuja kuona wapi tulikwama ili tukirudi katika
vikao vya bunge waweze kulipa msukumo wa kipekee ili mradi huu uweze kukamilika”
alisema Masauni
Akizungumza katika
ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Salum
Rehani amesema kamati imefuatilia mradi huo ambao umechukua muda mrefu bila
kukamilika na sasa kuna haja ya mradi huo kumaliziwa ili wananchi waweze
kufaidi matunda ya ulinzi na usalama.
“Kamati tumekuja kuona
mradi ulipogomea na tunashauri mradi huu umaliziwe haraka iwezekanavyo na kuna
msukumo maalumu tumepanga na mkandarasi lengo kituo hiki kikamilike maana
kubakia bila kukamilika mbeleni italeta matatizo,tunataka wananchi wa maeneo
haya wafanye shughuli zao za maendeleo wakiwa na huduma ya ulinzi na usalama ya
uhakika” alisema Rehani
Ujenzi wa jingo jipya
la Kituo cha Polisi Mkokotoni ulianzishwa baada ya jingo lililokuwa likitumika
kama kituo awali kuteketea katika tukio la ajali ya moto kutokana na hitilafu
ya umeme iliyosababishwa na miundombinu chakavu ya mfumo wa umeme iliyokuwa
katika jingo hilo baada ya kutofanyiwa ukarabati kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment