Mnufaika
wa Ruzuku inayotolewa na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), Bibi
Albina Matayo, mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Mtaa wa Mrara,
akitoa ushuhuda jana kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na
Serikali za Mitaa wa namna TASAF ilivyomuwezesha kuboresha maisha yake.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt.
Jasson Rweikiza (Mb), akieleza kuridhishwa na maendeleo ya Mnufaika wa
(TASAF), Bibi Albina Matayo, mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akishuhudia kokoto
zilizopondwa kwa ajili ya kuuzwa na Bibi Albina Matayo ambaye ni
Mnufaika wa Ruzuku inayotolewa na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
(TASAF), Halmashauri ya Mji wa Babati.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika picha na
mnufaika wa TASAF, Halmashauri ya Mji wa Babati, Bibi Albina Matayo
mbele ya nyumba iliyojengwa na mnufaika huyo kupitia Ruzuku inayotolewa
na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF).
Mbuzi
wanaofugwa na Bibi Albina Matayo, mkazi wa Halmashauri ya Mji wa
Babati, Mtaa wa Mrara ambaye ni mnufaika wa Ruzuku inayotolewa na Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), ambayo imemuwezesha kuwanunua mbuzi
hao.
James Mwanamyoto - Babati
Ruzuku inayotolewa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) kwa
mnufaika, Bibi Albina Matayo, mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Mtaa wa
Mrara, imemuwezesha mama huyo kuendesha biashara ya kuchakata kokoto na
kuziuza na hatimaye kuboresha maisha yake kwa kujenga nyumba bora ya bati,
ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto wake.
Bibi Matayo ametoa ushuhuda huo jana, mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo yenye
lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Manyara.
“Ruzuku yangu nimekuwa nikiitumia kupondaponda mawe ili kupata kokoto
ambazo nimekuwa nikiziuza kwa shilingi 80,000/= kwa lori moja na kuongeza
kuwa, ujira huo umemsaidia kujenga nyumba nzuri ya kuishi na familia yake,
kusomesha watoto wake na kufuga mbuzi” Bibi Matayo amefafanua.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za
Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb) amesema, kamati yake imejiridhisha
pasipo na shaka yoyote kuwa, TASAF imemuwezesha Bibi Matayo kuboresha
maisha yake, hivyo ameipongeza TASAF kwa kazi nzuri wanayoifanya ya
kuboresha maisha ya watanzania wenye kipato cha chini.
“Bibi Matayo anayo haki ya kutoa ushuhuda wa faida alizozipata kutokana na
TASAF kwani amejenga nyumba nzuri, iliyoezekwa vizuri kwa bati na ameweka
mfumo wa umeme kwenye nyumba yake hivyo anasubiria kuingiziwa umeme,”
Mhe. Rweikiza ameongeza.
Ruzuku inayotolewa na TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kiasi kikubwa imewawezesha wanufaika wa mpango huo, kuwekeza katika shughuli za
kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji wa kuku, bata, mbuzi, kondoo na kufanya
biashara ndogondogo za uuuzaji wa mbogamboga, kugonga kokoto na mama
lishe.

No comments:
Post a Comment