HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 15, 2020

LIPENI KODI YA ARDHI KWA WAKATI-LUKUVI

Na Lydia Lugakila, Kagera

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amewataka wakuu wa wilaya mkoani Kagera kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuhakikisha kila aliyemilikishwa ardhi kisheria analipa kodi ya ardhi kisheria kila mwaka.

Waziri William Lukuvi ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Kagera katika ziara ya siku moja iliyolenga kutatua changamoto mbali mbali zinazoikumba sekta ya ardhi mkoani Kagera.

Waziri Lukuvi amesema Mkoa wa Kagera umekuwa na changamoto mbalimbali za ardhi ikiwemo migogoro ya ardhi, muingiliano wa wageni mipakani,kiwango cha umilikishaji ardhi kuwa wa cha chini, muundo wa Wizara ya ardhi, usumbufu katika kufuatilia hati katika Mkoa wa Mwanza kwa kutumia gharama kubwa, pamoja na baadhi ya watendaji wa serikali kutokusanya kodi ya pango.

Waziri Lukuvi amesema licha ya changamoto hizo kuwepo mkoani Kagera lakini suala ukusanyaji wa kodi ya pango haufanyiki vizuri ambapo hadi sasa mkoa  huo upo chini ya 40%

Kufuatia hali hiyo Waziri Lukuvi amewataka wakuu wa wilaya mkoani humo kupanga mikakati ya pamoja ili kuhakikisha mwananchi aliyemilikishwa ardhi kisheria analipa kodi ya ardhi kisheria kila mwaka.

Ameeleza kuwa mtandao uliokamilika vijijini kama kuna wanaomiliki kwenye  vijini watumiwe watendaji wa vijiji wakusanye na mtandao wa watendaji wa mtaa na wapewe orodha ya kila mtaa ya watu waliomilikishwa ardhi kisheria ndani ya mtaa wao walipe kodi.

Amewahimiza wakurugenzi wanapanga bajeti ya kuvifikia vijiji ili kupanga mbinu bora ya ardhi ili kupunguza migogoro ya ardhi huku akisisitiza ardhi za vijiji kutouzwa hovyo hovyo.

Amesema kuwa Rais Magufuli amewakasimu madaraka ya kupanga ardhi lakini baadhi ya watu wamemwangusha kwani wanaowamilikisha ardhi wamekuwa hawalipi kodi ambapo wakurugenzi wametajwa kutoifanya badala yake usingizia maafisa ardhi.

Waziri huyo amesema hakuna Mkurugenzi katika Mkoa huo ambaye ameisha kusanya kodi kwa zaidi ya 40% ya bajeti ya mwaka huu.

Aidha amefanikiwa kutatua kero ya wananchi mkoani humo kufuatilia hati Mkoani Mwanza kwa gharama kubwa ambapo ofisi ya ardhi imerudishwa mkoani Kagera ambapo vifaa vya upimaji ardhi bure vitatolewa na watendaji kazi watawasili ili kufanikisha shughuli hiyo mkoani humo.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amempongeza Waziri Lukuvi kufika mkoani kwake na kutatua baadhi ya changamoto katika sekta hiyo na kumuhakikishia Waziri huyo kuwa Mkoa huo hautabaki kama ulivyo badala yake yatafanyika mapinduzi makubwa katika sekta ya ardhi na kuhakikisha mkoa huo unakuwa na msukumo wa juu ili kutimiza malengo tarajiwa.

Kikao hicho kimewashirikisha wakuu wa wilaya za mkoa wa Kagera, kamati ya ulinzi na usalama, wakurugenzi watendaji wa halmashauri, wataalam wa sekta ya ardhi.

No comments:

Post a Comment

Pages