Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akiongoza Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi
na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa
Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma.Aliyesimama
ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi, Ambayuu Kitiku.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akizungumza wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi
na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa
Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza, Suleiman Mzee akizungumza
wakati wa Kikao cha Makadirio ya
Mapato, Matumizi na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo
katika Ukumbi wa Makao Makuu ya wizara jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.
Mkurugenzi wa Sera na
Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Wanja Mtawazo akizungumza mbele ya Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi
na Miradi ya Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa
Makao Makuu ya wizara, jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha
Mipango wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ambayuu Kitiku akimpitisha katika randama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George
Simbachawene wakati wa Kikao cha Makadirio ya Mapato, Matumizi na Miradi ya
Maendeleo ya Jeshi la Magereza kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu
ya wizara, jijini Dodoma. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Jeshi la Magereza
nchini limedhamiria kuanzisha Kiwanda cha Mikate kitakachojengwa katika Chuo
cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga ili kwenda sambamba ya dhana ya Viwanda ya
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Hayo yamesemwa leo
Machi,20 na Mkuu wa Kitengo cha Mipango
wa Jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ambayuu Kitiku wakati akiwasilisha
maelezo ya Randama kuhusu Makadirio ya Mapato, Matumizi ya Kawaida na Miradi ya
Maendeleo kwa mwaka 2020/2021 mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George
Simbachawene wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
“Katika mpango wa
bajeti wa mwaka 2020/2021 Jeshi limeweka vipaumbele katika maeneo ya ajira na
maendeleo ya watumishi, utawala wa magereza, uboreshaji miundombinu ya majengo
ya magereza, kuimarisha shughuli za kilimo ili kujitosheleza kwa chakula, kuimarisha
shughuli za Shirika la Magereza na kuimarisha shughuli za Viwanda ikiwepo
Ujengaji wa Kiwanda cha Mikate kitakachojengwa katika Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji Ukonga kilichopo jijini Dar es Salaam” alisema SACP Kitiku
Akizungumza wakati
akichangia hoja hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene aliwataka
Jeshi la Magereza pindi mradi huo utakapoanza watengeneze mkate bora
wakizingatia suala nzima la masoko, teknolojia bora ikiwepo ladha ya mkate huo,
vifungashio vyake ili waweze kwenda sambamba na hitajio la mtumiaji wa mwisho
“Ni wazo zuri kwa
mlichopanga kwani mtakapofanikiwa mtakua mmeongeza kipato na ile dhana ya jeshi
la magereza kujitegemea itakua sasa imeingia kwenye utekelezaji sambamba na
kujitosheleza kwa chakula cha kulisha wafungwa, lakini katika mpango huo lazima
baadhi ya mambo muyafanyie utafiti ikiwepo soko linataka nini, teknolojia
mtakayotumia muhakikishe ni nzuri itakayowafanya mpate bidhaa yenye ladha nzuri
sambamba na kifungashio cha bidhaa hiyo, ni vizuri mmeliweka wazo wazi mapema
nadhani mtapata michango ya kuliboresha” alisema Simbachawene
Jeshi la Magereza
limeomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi 201,251.298,000/- katika mwaka wa
fedha 2020/2021 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo
huku likiweka lengo la kukusanya maduhuli ya Shilingi 2,000,000.000/- kwa mwaka
wa fedha wa 2020/2021.
No comments:
Post a Comment