Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wajumbe(hawapo pichani),
wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Kumi na Mbili
cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi ambapo amelitaka jeshi
hilo kuzingatia misingi ya sheria katika kudhibiti viashiria au matendo ya uhalifu
katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa
mwaka huu.Ufunguzi wa kikao hicho umefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa
wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro akizungumza
wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa
Idara ya Jeshi la Polisi ambapo ameahidi kupanga bajeti itakayosaidia kupambana
na changamoto mbalimbali kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Ufunguzi
wa kikao hicho umefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay
jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni.
Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro akitoa taarifa
ya ulinzi na usalama kwa nchi nzima mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),muda mfupi kabla ya naibu waziri kufungua Kikao
cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi,kilichofanyika
Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiweka saini katika daftari la wageni
baada ya kuwasili Bwalo la Maafisa wa Polisi,Oysterbay kufungua Kikao cha Kumi
na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi. (Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Na
Mwandishi Wetu
Serikali imelitaka
Jeshi la Polisi kuzingatia misingi ya sheria katika kudhibiti viashiria au
matendo ya uhalifu katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo
Machi 16,2020 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni
wakati akifungua Kikao cha Kumi na Mbili
cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi kilichofanyika katika
Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Napenda kuwapongeza
Jeshi la Polisi chini yako(IGP Sirro),kwa kufanikiwa kudhibiti matukio
mbalimbali ya uhalifu ikiwemo dawa za kulevya,ajali za barabarani na uhalifu
mwingine ambao hapo nyuma wote tulishuhudia ukiwa umeoata mizizi ila napenda
kutoa angalizo kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu mdhibiti viashiria vya
uhalifu au matendo ya uhalifu kwa kufuata misingi ya sheria ili tuweze kupita
kwa amani na salama katika kipindi hicho” alisema Masauni
Akizungumza katika
kikao hicho cha baraza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambae pia ni
Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro alisema wao kama jeshi wanaishukuru
serikali na wamejipanga kibajeti kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zozote
zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi
“Kwa kiasi tumefanikiwa
kutengeneza bajeti itakayochochea usalama wa raia na mali zao,bajeti
iliyoandaliwa itasaidia kutatua changamoto na kwa kuwa kila uchaguzi una
changamoto zake sisi tumejipanga na tunazichukua chgangamoto kama fursa”
alisema IGP Sirro
Watumishi hao wa Baraza
la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi wanakutana katika kikao hicho lengo
ni kujadili masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2019/2020
na Rasimu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2020/2021.
No comments:
Post a Comment