Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi, Betty Msimbe (kushoto), akimkabidhi msaada
wa vyakula mbalimbali, Lilian Mbise ambaye ni mlezi wa kituo cha kulelea watoto
yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu cha Sharom kilichopo katika
eneo la Kwa mathiasi kata ya Msangani
Wilayabi Kibaha,katika halfa iliyofanyika katika kituo hicho. (Picha na Victor Masangu).
Baadhi ya watoto yatima na wale wanaoishi
katika mazingira magumu katika kituo cha Sharom
wakiimba wimbo maalumu wakati wa hafLa ya kupokea msaada wa vvyakula mbalimbali.
Baadhi ya wanawake wanaounda kikundi cha Pwani
Generationi mwanamke sahihi wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi
katika mazingira magumu na yatima mara baada ya sherehe za kukabidhi vyakula
mbali mbali pamoja na mahitaji mengine ya msingvi katika kituo cha Sharom
kilichopo kata ya Msangani Wilayani Kibaha.
Mlezi wa wa kituo cha Sharom ambacho kinalelea
watoto yatima pamoja na wale amabo wanaishi katika mazingira magumu akipiga
makofi kwa furaha mara baaada ya kupokea msaada huo wa vyakula mbali mbali
pamoja na mahitaji mengine kutoka kwa kikundi cha Pwani Generation
mwanamke.
Mlezi wa kulelea watoto yatima na wanaosihi
katika mazingira magumu, Lilian Mbise, akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na kituo hicho cha Sharaom kilipotembelewa na kikundi cha Pwani
Generation mwanamke sahihi pamoja na kutoa shukrani zake za dhati kwa wanawake
hao wa Mkoa wa Pwani kuweza kwenda kuwatembelea na kuwafariji.
Mwenyekiti wa Kikundi cha PwaniGeneration
Mwanamke sahihi, Betty Msimbe, akizungumza na watoto yatima na wale wanaoishi
katika mazingira magumu hawapo picha wakati wa sherehe hizo za kutoa msaada wa
mahitaji mbali mbali ikiwemo vyakula.
Baadhi ya wanawake wanaounda kikundi cha Pwani
Generationi mwanamke sahihi wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi
katika mazingira magumu na yatima mara baada ya sherehe za kukabidhi vyakula
mbalimbali pamoja na mahitaji mengine ya msingi katika kituo cha Sharom
kilichopo kata ya Msangani Wilayani Kibaha.
Na Victor Masangu,
Kibaha
Watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu katika
kituo cha Sharom kilichopo kata ya
Msangani Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli
kuwasaidia kwa hali na mali kuwasaidia kuwatatulia
changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa mahitaji ya chakulai,nguo, huduma
za matibabu pamoja na ujenzi wa jengo la nyumba kwa ajili ya kuweza kuishi.
Baadhi ya watoto hao akiwemo Sara Yendemba Dickson Michael na wakizungumza
wakati wa halfa ya kupokea msaada wa mahitaji mbali mbali ikiwemo chakula
kutoka kwa kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi walisema kwamba baada
ya kuondokewa na wazazi wao wamekuwa wanaishi katika mazingira magumu na wakati mwingine walikuwa wanakwenda
kutafuta chakula majalalani hivyo wanahitaji msaada wa hali na mali kutoka
serikalini na wadau wengine wa maendeleo ili waweze kujikimu kimasiha kama
watoto wengine.
“Tunashukuru sana kwa msaada wa vyakula mbali mbali ambavyo
tumepatiwa na uongozi wa wanawake wa Pwani Generation kwani utaweza
kutusaidia kwani sisi hapa ni watoto yatima na wengine tunaishi katika
mazingira magumu, lakini kitu kikutu bado tunamuomba Rais wetu aweze kutusaidia
zaidi ujenzi wa nyumba ya kulala kwani idadi yetu ni kubwa kuliko vitanda
vilivyopo”walisema watoto hao kwa masikitiko makubwa.
Pia waliongeza kwamba kabla ya kufikishwa katika kituo hicho
walikuwa wanaishi mitaani kwa shida kubwa sana kutokana na kukabiliwa na
changamoto mbali mbali ya kukosa mavazi, chakula sambamba na mambo mengine
muhimu lakini kutokana na kituo hicho angalau wameweza kupatiwa hata fursa ya
kwenda shule ya ajili ya kupata elimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation
mwanamke sahihi, Betty Msimbe, amesema kwamba wameamua kutoa msaada huo wa
mchele, mafuta, unga, sukari, pamoja na maharage katika kituo hicho kutokana na
kubaini kuwepo kwa changamoto nyingi ambazo zinawakabili watoto hao ambao
wanahitaji kusaidiwa mahitaji mbali mbali ili weze kujikimu kimaisha.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba katika kikundi chao wamekuwa
na utaratibu wa mara kwa mara kwenda kutoa misaada katika vituo mbali mbali vya
kulelea watoto yatima na wale wanaosihi katika mazingira magumu vilivyopo
katika Mkoa wa Pwani lengo ni kuwapatia
mahitaji muhimu ambayo wanastahili pamoja kwenda kuwafariji.
“Sisi kama Pwani Generation mwanamke sahihi tumeweza kubaini
kuwa kituo hiki cha Sharom ambacho kipo katika Wilaya ya Kibaha bado
kinakabiliwa na changamoto mbali mbali na ndio maana tukaamua kujikusanya fedha
na kuamua kununua mahitaji mbali mbali ambayo wanastahili kupatiwa watoto hao
kwani kutoa ni moyo na wala sio utajiri hivyo ni moja ya kuunga mkoni juhudi za
serikali katika kuwasaidia watoto,”alisema Msimbe.
Naye mlezi wa Kituo hicho Lilian Mbise ambaye pia na yeye ni yatima amesema kwamba kituo hicho ambacho
kilianzshiwa tangu mnamo mwaka 2016 kina watoto wapatao 18 ambao wanaishi
katika nyumba ya kupanga hivyo kunahitajika msaada zaidi kutoka serikalini kwa lengo la kuweza
kuzitatua changamoto hizo zinazowakabili kwani mahitaji yao ni mengi.
Kikundi hicho cha Pwani Generation mwanamke sahihi kilitoa
msaada wa vitu mbali mbali mbali ikiwemo unga wa sembe, sukari, mafuta ya kula,
mchele,maji pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa ajili ya watoto yatima na
wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Sharoom ambapo vimegharimua
kiasi cha zaidi ya shilingi milioni moja.
No comments:
Post a Comment