Spika wa
Bunge, Job Ndugai (Mb), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadiliko
ambayo yatafanyika katika Utaratibu wa
Uendeshaji wa Shughuli za Bunge wakati wa Mkutano wa Bunge wa Bajeti
unaotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma. Mheshimiwa Spika ametangaza mabadiliko
kadhaa ambayo yatafanyika wakati wa uendeshaji wa shughuli za Bunge ili
kukabiliana na janga la Ugojwa wa Korona. Wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati)
akizungumza wakati wa Kikao cha kamati ya Uongozi ambayo ilikutana ili kujadili
na kupitisha shughuli zitakazofanyika wakati Bunge la Bajeti linalotarajiwa
kuanza kesho Jijini Dodoma. kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson
na Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akizungumza
wakati wa Kikao cha kamati ya Uongozi ambayo ilikutana ili kujadili na
kupitisha shughuli zitakazofanyika wakati wa Bunge la Bajeti linalotarajiwa
kuanza kesho Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai na Kulia
ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Jenista Mhagama.
Wajumbe wa kamati ya Uongozi katika kikao
cha Kamati kilichokutana ili kujadili na kupitisha shughuli zitakazofanyika
wakati wa Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza kesho Jijini Dodoma. (Picha na Bunge).
No comments:
Post a Comment