HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 06, 2020

NMB yakabidhi vifaa kwa Wilaya ya Hai na Ilala

BENKI ya NMB imekabidhi misaada mbalimbali ya vifaa tiba na vifaa vya elimu katika mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kurejesha kwa jamii asilimia moja ya faida yao kupitia Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

 Jijini Dar es Salaam, NMB imetoa msaada yenye thamani ya Sh. Milioni. 15 kwa Shule ya Sekondari Tambaza, iliyopo Upanga na Kituo cha Afya Pugu Kajiungeni wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, wakati Mkoani Kilimanjaro imekabidhi vifaa tiba kwa Hospitali ya Wilaya ya Hai.

Tambaza Sekondari, imepokea msaada wa vitanda 80 vya kulalia wasichana wa shule hiyo vyenye thamani ya Sh. Mil. 10, vilivyokabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd na kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Zungu.

Katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba katika Kituo cha Afya Pugu Kajiungeni, NMB ilikabidhi msaada huo wenye thamani ya Sh. Mil. 5 kupitia kwa Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo cha Biashara za Serikali, Adelard Mangombo, na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Sofia Mjema. 
NMB Karibu Yako.
Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo cha Biashara za Serikali -  Adelard Mang'ombo akimkabidhi msaada wa vifaa vya afya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema, ambavyo ni vitanda vitano pamoja na mashuka katika Kituo cha Afya Pungu Kajungeni vyote vyenye thamani ya Sh. Milioni 5.
Mkoani Kilimanjaro, NMB kupitia Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro, alikabdhi msaada wa vitanda vitano vya kulalia, viwili vya kujifungulia akina mama, mashuka 25, magodoro 5 pamoja na hundi ya Sh. Milioni 16 kwa ajili ya wakulima wa zao la vanilla mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Pages