HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2020

MAAFISA TARAFA KAGERA WAPEWA PIKIPIKI

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Generali Marco Gaguti, akikabidhi pikipiki kwa maafisa Tarafa walioko mipakani.


Na Alodia Dominick, Bukoba

Pikipiki zenye thamani ya shilingi milioni 11.5 zimegawiwa kwa maafisa tarafa wanne mkoani Kagera ambao tarafa zao ziko maeneo ya mipakani ili kuwaongezea ufanisi wa kazi za kila siku.

Pikipiki hizo aina ya sh/nerey zimegawiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia generali Marco Gaguti baada ya kuzindua baraza la wafanyakazi mkoa wa Kagera.

Maafisa Tarafa waliopokea pikipiki ni Afisa tarafa ya Murongo wilayani Kyerwa, Tarafa ya Murusagamba wilaya ya Ngara, Tarafa ya Kiziba wilaya ya Misenyi na tarafa ya Nshamba wilaya ya Muleba.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti baada ya kuzindua baraza la wafanyakazi mkoa wa Kagera amekabidhi pikipiki nne kwa maafisa tarafa mkoani humo.

Akikabidhi pikipiki hizo amesema ni imani yake kuwa kutokana na changamoto zilizopo kwenye kata hizo basi baada ya kupatikana usafiri zitaweza kupungua na kuwa wazitunze na wazitumie pikipiki hizo kwa shughuli zilizokusudiwa kwa kuondoa changamoto ya magendo ya kahawa maeneo ya mipakani.

Afisa tarafa wa Nshamba wilayani  Muleba Clementina Msafiriameshukuru kwa kupewa  pikipiki hiyo na kuahidi kuitunza na kwamba ni chombo ambacho kitarahisisha shughuli za kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo kufuatilia wanaovusha magendo ya kahawa.

Katibu Tawala mkoa wa Kagera, Faustine Kamzora, amesema kuzinduliwa kwa baraza hilo ni kutoa nafasi ili baraza liweze kuelezea changamoto zinazowakumba wafanyakazi ikiwemo kuwataka waajiri kuwalipa  watumishi wanaodai ni pamoja na baraza kushiriki katika kupitisha bajeti.

Ikumbukwe kuwa, pikipiki hizo zimetolewa msaada na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA na mkoa kuwapatia maafisa tarafa ambao wana changamoto nyingi na hasa tarafa za maeneo ya mipakani.

No comments:

Post a Comment

Pages