HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 06, 2020

ZANZIBAR YAZUIA NDEGE KUTOKA ITALIA KUHOFIA VIRUSI VYA CORONA

Na Talib Ussi, Zanzibar 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imezuia mashirika yote ya ndege yanayosafirisha watalii kutoka Italia kuja Zanzibar kama njia moja ya kuzuia maradhi ya Corona Visiwani humu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Muhammed, hapo wizarani kwake Mnazi mmoja na kueleza zuio  hilo litaendelea mpaka pale watakapojiridhisha uwepo ugonjwa huo nchini Italiya.

Alisema serikali imefikia maamuzi hayo kutokana hali ya maradhi hayo nchini humo.

Alisema nchi hiyo ni ya pili baada ya china kwa maambukizi lakini watalii wengine wanaoingia zanzibar ni Wataliana .

"Wachina wanakuja hapa lakini woote ni wataalamu wa afya miradi wanapokuja huwekwa kwenye kambi maalum kwa siku 14 kama wakionekana salama hurusuwa kufanya shuhuli zao" alisema waziri Hamad.

Hamad alieleza kuwa yuko mtaliana  mmoja alikuwepo Zanzibar na kuondoka kurudi kwao na kuoneka na maradhi hayo.

"Tunafuatilia kwa karibu kujua nchi gani alipita mtalii huyo mpaka kufika kwa sababu kwetu hadi leo tunatamka hatuna ugonjwa huo" alisema Hamad.

Sambamba na hilo waziri huyo alisema hadi sasa hakuna chanjo ya maradhi hayo  na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wowote.

Alieleza katika kujikinga na ugonjwa huo usiingie nchini aliwataka wazanzibari kama hakuna ulazima hakuna haja ya kusafiri katika nchi ambazo zimekumbwa na Ugonjwa huo.

"Kwa sababu hili ni jukumu letu sote kuhakikisha maradhi hayaingii kwetu basi mmoja achukue hatua" alieleza Hamad.

Kwa upande wake Mkurugenzi Kinga wizara hiyo Dk. Fadhili Muhamed aliwataka wananchi kuwa na utamaduni wa kuosha mikono kila wakati na kuwaomba yeyote atakayehisi mafia makali afike hospital kwa ajili matibabu.

Dk. Fadhili alisema Wazara katika kukabiliana na maradhi hayo tayari imetenga maneno maalum kama akipokea mgonjwa wa aina atawekwa huko

No comments:

Post a Comment

Pages