Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Sweetbert Njewike, akizungumza na waandishi wa habari kukanusha kuwepo kwa mauaji wilayani Manyoni.
Waandishi wa habari mjini hapa wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari mjini hapa wakichukua taarifa hiyo.
Na Ismail Luhamba, Singida
JESHI la Polisi Mkoa wa Singida limewataka wananchi kupuuza habari zinazozagaa mitandaoni zinazodaiwa watu 14 wamekufa kwa kuchinjwa wilayani Manyoni.
Akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Sweetbert Njewike amesema taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini , Godbless Lema ni ya uongo yenye lengo la kuleta taharuki kwa wananchi.
‘’ Lema alitoa taarifa hiyo wakati akitoa salamu kwenye msiba wa Alex Jonas ambaye alikutwa ameuwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake katika eneo la Mbungani, ambapo alionyesha orodha ya watu 14 akidai waliuwa kwa kuchinjwa wilayani manyoni,bila ya kuwa na uhakika kama taarifa hizo ni sahihi, na kulituhumu jeshi la polisi mkoa wa Singida kuwa limeshindwa kutekeleza wajibu wake” alisema Njewike.
Aidha Njewike alisema kuwa matukio yote ya mauaji yaliyotolewa na Mbunge huyo yametokana na wizi,wivu wa mapenzi na migogoro ya kifamilia na kuongeza kuwa wamefungua jalada la uchunguzi, dhidi ya mbunge huyo, uchunguzi ukikamilika watachukua hatua za kisheria dhidi yake.
No comments:
Post a Comment