Na Asha Mwakyonde
MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko amesema kuwa ofisi yake imepunguza bei za usajili wa kemikali na maeneo ya kuzalishia bidhaa kwa wajasiriamali wadogo lengo likiwa ni kuwafanya wajasiriamali hao wajisajili kwa wingi toafauti na awali.
Awali kemikali moja ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 40,000 ambapo kwa sasa imepungwazwa hadi kufikia 10,000 na eneo la kuzalishia 50,000.
Akizungumza Machi 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya wajasiriamali 176 waliohitimu mafinzo hayo ya usimamizi wa usalama wa kemikali , Dk. Mafumiko, amesema kilio kikubwa cha wajasiriamali ni bei kubwa za za uzajili wa kemikali na kampuni.
Amesema mtumiaji yeyote wa kemikali lazima ajisajili na kwamba awali wajasiriamsli hao wslikuwa wanaona usajili ni gharama, hivyo ofisi yake imepunguza.
Dk. Mafumiko aliongeza kuwa Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa serikali ndiyo msimamizi wa Kemikali, ambapo kwa mujibu wa sheria mtu anayejihusisha na kemikali kwa kuuza, kutumia, kuingiza kutoka nje ya nchi au kutoa lazima asajiliwe na Mkemia Mkuu wa serikali.
Amesema kusajiliwa kunaambatana na kupewa cheti ambacho kinaruhusu kufanya shughuli za kutumia kemikali.
Ameeleza kuwa kemikali zinafaida kubwa katika kutengeneza bidhaa mbalimbali kwenye viwanda lakini zipo ambazo ni bashirifu kwani zikitumika tofauti zinaweza kutumika kama dawa za kulevya.
“Kemikali hizi zikichepushwa kwenye matumizi ambayo si sahihi zinaweza kuharibu afya zikitumika kama dawa za kulevya hasa kwa vijana,”amesema.
Amewaonya vijana kubadili tabia na kuacha kutumia kemikali kwani ikiingia mwilini kutoka inatumia muda na gharama kuwa kubwa hivyo watumie kwa ajili ya kujiongezea kipatao na uchumi wa nchi.
Aidha baadhi ya wajasiliamali hao walishukuru kwa kupata mafunzo hayo ambayo ni muhimu kwao pamoja na kupunguziwa gharama za usajili wa kemikali moja.
Naye mjasiriamali Nazael Brown amesema ameelimika namna ya kutumia na kujikinga na matumizi ya kemikali ambazo ni hatari kwa afya yake.
“Mafunzo yametuelimisha namna ya kutumia kemikali ambazo ni hatari kwa afya ya binadamu, lakini yametolewa kwa muda mfupi kwani yanahitaji muda wa kutosha kutokana na zile kemikali zinaathiri afya ya binadamu,”amesema.
Ameongeza kuwa wapo watu ambao kufundishwa kwao kunachukua muda mrefu kuelewa hivyo kwa siku moja pekee hakutoshi.
No comments:
Post a Comment