Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu akitoa Elimu ya
Ugonjwa wa Corona (Covid -19) Kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya
dini (Hawapo pichani).
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini katika mkoa wa Rukwa wakiiombea
nchi kuepukana na ugonjwa wa Corona (Covid-19) mara baada ya kumaliza
kikao kilichoitishwa na mkuu wa mkoa wa Rukwa.
Na Mwandishi Wetu
Viongozi wa
madhehebu ya dini mkoani Rukwa wamekubaliana kuwa kila dhehebu kulingana na
imani zao kuona namna ya kupunguza muda wa kufanya ibada katika misikiti na makanisa
mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na
virusi vya Corona (Covid-19).
Wamekubaliana
hayo wakati wa kikao kifupi kilichoitishwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura katika
kikao hicho kilicholenga kuwaelimisha viongozi hao juu ya Chanzo, usambaaji na
namna ya kujikinga na ugonjwa huo ambao unaendelea kuisumbua dunia huku jukumu
la kutoa elimu likifanywa na Mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa.
Wakati
akielezea namna ya kutekeleza azma hiyo Shekhe wa mkoa wa Rukwa Rashid
Akilimali alisema kuwa atazungumza na mashekhe wa wilaya na Maimamu wa miskiti
ya mkoa huo kupunguza muda wa ibada ili kukwepa kuwaweka watu wengi katika eneo
moja kwa muda mrefu lakini pia kuwafanya waumini hao wasikose ibada hizo.
“Niungane na
Askofu wa Monravian, tupunguze nyakati za ibada zetu, na kubwa iwe ni kuongoza
dua na maombi kwaajili ya nchi yetu, sisi tumelipunguza hili baada ya kutokea
hili, ibada ya nusu saa tumekwenda dakika kumi na tano, dakika kumi inakuwa ni
mahubiri na dakika tano ni kuiombea nchi ili Mungu atuepushe na jambo hili,” alisema
Naye Mwakilishi
wa Kanisa la Anglikan Mkoani Rukwa Mchungaji Mathias Gwakila alisema kuwa
atajitahidi kufikisha ujumbe na elimu aliyoipata kutokana na namna
alivyojifunza na kuwasisitiza waumini hao kuendelea kufanya maombi ili
kuepukana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa ugonjwa huo ni pepo na hivyo
hatunabudi kulikemea na kisha kushauri juu ya kufupisha ibada.
“Hicho ni
kitu muhimu mno, ibada ziwe fupi zisiwe ndefu, kwahiyo kwa ushauri wangu
kupitia madhehebu mengine yote, viongozi wote wa madhehebu wajitahidi kufupiza,
kwa mfano kanisa la Anglican ibada zetu ni masaa mawili, sasa tufupishe, ibada
ichukue saa moja katika vipengele vyovyote vile ambavyo wewe utaviona upunguze
kipi na kipi ilimradi ibada iwe fupi watu watoke mapema,” Alisema.
Kwa upande
wake Mwakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Ziwa Tanganyika
Mchungaji Haruni Kikiwa alisema kuwa kupitia kikao hicho wamepata elimu ya
kutosha ya namna ya kuwaelekeza wananchi ambao ni waumini wao juu ya namna ya
kupambana na janga la kirusi cha Corona na kusisitiza kuwa atayafikisha kwa
askofu ili kusambazwa kwa makanisa.
“Tunachukua
hatua za kunawa kabla ya ibada na baada ya ibada, lakini pia hatua za kupunguza
muda wa ibada ili kupunguza muda wa waumini kukaa pamoja katika msongamano
lakini pia hatua za kupunguza misongamano kwa makanisa makubwa kwa maana
wanaweza wakafanyia hata nje ili kupunguza msongamano watu wakae mbalimbali,
haya yote nitayafikisha,” alisema.
Kwa upande
wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu wakati akieleza namna
ya kujikinga na ugonjwa huo alitoa msisitizo kwa viongozi hao kutumia maji
tiririka pamoja na sabuni ya maji wakati wa kunawa huku akieleza madhara ya
kutumia sabuni ya unga na ya kipande kuwa na tabia ya kushikwa na kila
mtumiaji.
“Sabuni ya
unga ambayo imechanganywa na maji ikawekwa kwenye chombo maalum kama chupa,
kwahiyo mtu anaweza kuitumia hii, tunaepuka kuweka sabuni ya unga kama ilivyo
kwamba mtu mmoja achukue na mwingine aje achukue na mwingine achukue, tunaepuka
kuweka sabuni ya kipande kwasababu lazima mtu aje aishike akishajipaka arudishe
mwengine aje aishike, kwahiyo tunasema ni sabuni ya maji na kama ni sabuni ya
unga basi ichanganywe na maji,” Alisisitiza.
Wakati
akifunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura aliwaomba
viongozi hao kuzingatia makubaliano ya kikao hicho na kuongeza kuwa anaamini
viongozi wa dini wasingependa waumini wao wateketee na kisha kusisitiza juu ya
kupunguza muda wa ibada pamoja na mikusanyiko hasa kwa madhehebu ambayo yana
waumini wengi.
“Kuna
makanisa ambayo ni madogo sana au misikiti midogo watu wanajua lakini kama
mikiti naona wameshajipanga wao wanasali muda mfupi lakini kuna makanisa
mengine tunatumia masaa mengi, mkishaingia saa 4 mpaka saa 9 kwahiyo huo ni
muda mrefu sana mnaweza mkajichanganya sana, hivyo ninaona kwamba hii
kumbunguza mud ani muhimu zaidi, vile vipindi vyetu tuvipunguze zaidi tutoe
elimu hasa ya kuwa na imani,” Alisistiza
Aidha,
alibainisha kuwa kama serikali hawataweza kuwapangia muda wa kufanya inbada
hizo huku akiweka msisitizo kuwa imani zinatofautiana na kufafanua kuwa waumini
hao wanaweza hata kulala ndani ya makanisa yao kwa kuomba lakini msisitizo ni
kuwa wachache ili kuepusha msongamano.
No comments:
Post a Comment