HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 08, 2020

Wanawake katika kipindi cha serikali ya awamu ya Tano wamefanya vizuri na kubaki katika nafasi zao kuliko Akina Baba –Katibu Tawala Makame

*THTU yataka wanawake kufanya kazi kwa umahiri pindi wanapopata nafasi

*Maafisa Rasilimali watakiwa kufuata sheria za upandishaji Vyeo


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 


 Wanawake  wengi waliopata nafasi wameonyesha uwezo wa kufanya vizuri hali ambayo imefanya kubaki katika nafasi zao ikilinganishwa na wanaume kwa kipindi cha miaka mitano.

Hayo aliysema Katibu wa Tawala Wilaya Ilala Jabir Makame katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kwa Chuo cha Biashara (CBE). Makame ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema amesema Wanawake ni wana uthubutu katika kufanya Kazi.

Amesema kwa mwaka huu wa uchaguzi Wanawake watumie nafasi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuweza kuingia kwenye kufanya maamuzi.

Maadhinisho hayo yaliratibiwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa Kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU).

Amesema Serikali imeweka mazingira mazuri kwa Wanawake kwa kuwepo kwa Makamu wa Rais pamoja ngazi mbalimbali za uongozi wanawake wapo.

Aidha amesema serikali imeweka mazingira ya kuwepo kwa mikopo ya Wanawake na fedha zipo na kutaka  wanawake kwa kuendeleo imara kwa kuwa wazalishaji mali pamoja.

Kwa upande wa  Mwenyekiti wa  Kamati ya Wanawake  Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU)  Salma Fundi amesema kuwa THTU inatambua serikali imetunga sheria, miongozo na kanuni  ambazo kama zingetekelezwa vizuri basi tunauhakika asilimia 70  ya matatizo au kero za Wafanyakazi zingeweza kupungua na baadhi ya kero  kuisha kabisa.

Amesema kuwa kuna   ucheleweshaji wa Kupandishwa Madaraja kutokana na uzembe na ushauri mbaya kwa waajiri kutoka kwa  bàadhi Maafisa Rasilimali Watu kutowapandisha watu kwa wakati kwenye mfumo wa LOWSON pindi mtu anapofikisha sifa za kupandishwa, yaani miaka minne lakini mafanyakazi huyo anaweza kubaki kwenye cheo kimoja kwa miaka mingi bila kupandishwa  wakati miongozo ipo .

Fundi amesema kuna upendeleo au ubaguzi,  kupandisha watu vyeo, na wakati mwingine kuwapandisha watu  bila kuwaingiza kwenye bajeti za vyuo, kutokupandisha malimbikizo ya watu kwenye mfumo wa LOWSON kwa wakati na kufanya watu wakose malipo hayo, kutoa vyeo vya kukaimisha bila kufuata utaratibu na kuwafanya watu wakose haki zao, kushindwa kutekeleza Waraka wa Msajili wa Mwaka 2015 ambao unaelekeza haki ya mtu kuombewa tofauti ya mshahara wake wa awali kama mshahara binafsi na kusababisha manunguniko mengi.

“ Alitoa wito Wanawake kuacha kurudi nyuma na kusema Uongozi ni Kazi za Wanaume wakati uwezo wa kufanya wanao. chukueni  fursa zilizopo, ni Haki yetu ikiwemo kugombea nafasi za Uongozi wa Siasa katika Mwaka huu wa Uchaguzi. 


Mwisho nawakumbusha wanawake kama tunataka kufikia hamsini kwa hamsini tusisahau kuwawezesha wanawake wenzetu Kama tukiweza kufanya kila mwanamke kiongozi asaidie kunyanyua mwanamke mmoja au wawili kushika madaraka basi tutaweza. Walimaliza kwa kusema wanawatakia  maadhimisho mema wanawake wote na kuwaombea kwa kusema anawapenda sana wanawake wote na Mungu Aibariki Tanzania, Mungu Awabariki Wanawake Wote”. Amesema Fundi.
 Katibu Tawala wa Manispaa ya Ilala Jabiri Makame akizungumza  katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani kwa Wafanyakazi wanawake wa Chuo cha Biashara  (CBE) kwa  na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU)  maadhmisho yalifanyika katika wa Chuo cha Biashara  (CBE) jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa  Kamati ya Wanawake  Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU)  Salma Fundi  akizungumza na wafanyakazi wanawake wa Chuo cha Biashara  (CBE) kuhusiana masuala ya wanawake na changamoto katika ajira.
 akamu Mkuu wa Chuo  Taaluma wa Chuo cha Biashara (CBE)  Profesa Edda Luoga akizungumza kuhusiana na wanawake wanavyotoa mchango katika maendeleo katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yalifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Kamati ya wanawake Taifa wa wanachama wa Chama ambao ni wanawake wa wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU) Roselyne Masam akisoma lisala kwa mgeni rasimu kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wanawake duninia kwa chuo cha Biashara (CBE).
 Maadhinisho ya Siku ya Wanawake wakiimba wimbo wa mshikamano.
Baadhi ya Wanawake THTU wakiwa katika maadhinisho katika chuo Cha Biashara (CBE).

No comments:

Post a Comment

Pages