WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi matreka 19 yenye thamani ya sh. bilioni
1.520 yaliyotolewa kwa mkopo na Benki za NMB na CRDB kwa ajili ya
wakulima wa mkonge wanaounda Vyama vya Msingi (AMCOS) vinne vya kilimo
cha mkonge.
Ameyasema hayo leo(Alhamisi,
Machi 5, 2020) baada ya kutembelea eneo eneo la shamba la mkonge la
wakulima wadogo Mwelya Sisal Estate na kujionea shughuli za za
usindikaji mkonge na kukabidhi matrekta kwa wakulima.
Benki
ya NMB imetoa matrekta 11 na matera 22 yenye thamani ya sh. bilioni
moja na CRDB imetoa matrekta manane na majembe yake yenye thamani y ash.
milioni 520.
Waziri
Mkuu amesema zao la katani ni miongoni mwa mazao saba ya biashara
nchini, hivyo amewahamasisha wananchi kulima zao hilo kwa wingi.
“Maafisa kilimo hakikisheni mnawasaidia wakulima kuanzia hatua za awali
za utayarishaji shama hadi mavuno hadi utafutaji wa masoko.”
Amesema
lazima zao hilo liuzwe kwa mfumo wa ushirika, wanatambua kuna wakulima
wakubwa, wadogo na wa kati wote wanatakiwa waratibiwe vizuri ili
wanaohitaji waende kununua kwa mfumo huo na namna ya kuuza iwe ya
ushindani.
Pia,
Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote inayolima zao la mkonge
waratibu na kuwatambua wakulima wote katika maeneo yao wawasajili na
kuwaunganisha katika ushirika ambao utasaidia katika kuwapa elimu na
namna bora kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kupata pembejeo na zana za
kilimo.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amezipongeza benki kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya
kuwasaidia wakulima kwa kuwakopesha matrekta ambayo yatarahisha shughuli
za kilimo cha zao hilo la mkonge.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa AMCOS wahakikishe
wanatoa taarifa za mapato na matumizi kwa wanachama wao na pia hata
wanapokopa mikopo wawajulishe wanachama na wasitumie vibaya madaraka yao
na kula mali za ushirika.
Amesema
vyama vingi vya ushirika vimekufa kutokana na kuwa na viongozi
wasiokuwa waaminifu wanaoshiriki katika kufuja mali za ushirika.
“Serikali itawafikisha mahakamani viongozi wote wa ushirika wasiokuwa
waaminifu.”
“Viongozi
kama mnafikiria kwenda kwenye ushirika kwa ajili ya kuondoa umasikini
usichukue fomu na kama upo madarakani andika barua ya kujiuzulu leo.
Tutafanya uchunguzi na tukikubaini tutakupeleka mahakamani, hatuna mzaha
na fedha za wananchi. Tumedhamiria kurugudisha ushirika wenye tija kwa
wananchi.”
Kwa upande wake,Naibu
Waziri wa Kilimo Omar Mgumba amesema awali mashamba hayo manane ya
mkonge yalikuwa yanamilikiwa na Serikali na kisha waliyabinafsisha
matatu na matano yakabakia chini ya Bodi ya Mkonge.
Naibu
Waziri huyo amesema Bodi ya Mkonge waliwapa wakulima wadogo
wayaendeleze lakini kwa kipindi chote cha miaka 14 kuanzia 2004 hadi
2018 walikuwa wanalima na mapato yote yalikuwa yakwenda kwa muwekezaji
kutokana na mfumo uliokuwepo.
Naye,Mweyekiti
wa Wenyeviti wa AMCOS za zao la mkonge mkoani Tanga za mashamba ya
Magoma, Magunga, Mwelya, Hale na Ngombezi, Bw. AmGreyson Nnyari amesema
AMCOS zao zina jumla ya wanachama 1,081.
Amesema
kilimo cha mkonge kwa kuwashirikisha wakulima wadogo kilianza 1999
katika shamba la Mwelya na kuenea kwenye mashamba yay a Magoma, Magunga,
Ngombezi na Hale ilipofika 2002 na muasisi wa mfumo huo ilikuwa Kampuni
ya Katani Limited.
“Baada
ya kampuni ya Katani Limited kuendesha mfumo huo kwa miaka 14
malalamiko mengi yalijitokeza kutoka kwa wakulima na kuonesha kuwa mfumo
huo haukuwa rafiki kwa sababu mkulima alikuwa analipwa kiasi kidogo na
fedha na kwa wakati anaotaka yeye licha ya mkulima kusimamia shughuli
zote za shamba kuanzia hatua na uuandaji, upandaji, uvunaji na
usafirishaji wa mkonge hadi kiwandani.”
Amesema
baada ya malalamiko hayo ya wakulima kufikishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Bw. Martine Shigela aliunda kikosi kazi ambacho kilijumuisha Bodi
ya Mkonge na Halmashauri ya wilaya ya Korogwe ili kubaini ukweli wa
madai ya wakulima.
Bw.
Nnyari amesema baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi hicho
ni pamoja na kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa kilimo hicho kwa
wakulima wadogo na kuagiza Mkaguzi Mkuu wa Heshabu za Serikali kufanya
uhakiki wa kubaini uhalali wa madeni yote ambayo kampuni ya Katani
inadaiwa na ambayo inawadai wakulima.
“Baada
ya uchunguzi huo Serikali ilibaini kwamba Kampuni ya Katani Limited
iliwapunja wakulima kuanzia 2008 hadi 2018 jumla ya sh. bilioni 29.4
ambazo ni pamoja na fedha za SACCOS na AMCOS. Aidha wakulima nao
walikuwa wanadaiwa kiasi cha sh. bilioni 2.8.”
Amesema
Desemba 2018 Serikali ilifanya mabadiliko kwa kuiondoa Kampuni ya
Katani Limited katika shughuli za wakulima na kuipa AMCOS kazi ya
kusimamia shughuli zote kuanzia utayarishaji wa mashamba, uvunaji na
uuzwaji ambao kwa sasa unafanyika kwa kupitia minada na mnunuzi
anapatikana kwa njia ya ushindani tofauti na awali ambapo kampuni ya
katani ilikuwa mnunuzi pekee.
Mwenyekiti
huyo ametaja mafanikio yaliyopatikana baada ya AMCOS kupewa uendeshaji
wa mashamba hayo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapato ya mkulima
kutoka sh. 206,000 kwa tani moja hadi kufikia sh. milioni 1.450.
No comments:
Post a Comment