*Benki ya CRDB yatoa Sh. Milioni 210

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakipokea
mfano wa hundi yenye thamani ya Sh.Milioni 150 kutoka kwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Benki ya CRDB, Dk. Ally Laay (wa pili kulia) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ikiwa ni mchango kwa
Serikali dhidi ya mapambano ya virusi vya Corona (COVID-19). (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa amepokea msaada wa fedha pamoja na vitu mbali mbali kwa ajili ya
kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya
corona (COVID-19) wenye thamani ya sh. bilioni 1.185 kutoka kwa wadau.
Amewataka Watanzania
wote waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ili kuzuia usisambae
zaidi nchini. “Hii ni vita kubwa inahitaji tupigane kwa lengo la kuzuia janga
hili lisisambae zaidi nchini, hivyo tuzingatie maagizo ya Mheshimiwa Rais Dkt.
John Pombe Magufuli ya kumtaka kila Mtanzania ashiriki kwenye vita hii”
Amepokea msaada huo
leo (Jumamosi, Machi 28, 2020) katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Magogoni,
jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amewashukuru wadau hao na kuwataka Watanzania
waendelee kushirikiana na Serikali katika hatua zinazochukuliwa kukabiliana na
ugonjwa huo.
Miongoni mwa wadau
waliotoa msaada huo ni taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya CRDB iliyotoa Sh. Milioni 150 ikiwa tayari ilishatoa msaada wa Sh. Milioni 60 kwa Hospitali ya Mount Meru, Arusha na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), ambapo benki hiyo imetoa jumla ya Sh. Milioni 210 kwa ajili ya mapambano ya virusi vya corona, UBA Tanzania imetoa Sh. Milioni 230 na NMB Sh. Milioni 100.
Wadau wengine ni Karimjee Jivanjee Ltd na kampuni zake tanzu waliotoa sh. milioni 200 pamoja na kuhaidi kufanyia matengenezo kinga ya magari yote ya Toyota yanayotumika katika kukabiliana na COVID-19 kwa muda ya siku saba bure, Familia ya Karimjee imetoa jenereta la KVA 180 lenye thamani ya sh. milioni 75.
Wadau wengine ni Karimjee Jivanjee Ltd na kampuni zake tanzu waliotoa sh. milioni 200 pamoja na kuhaidi kufanyia matengenezo kinga ya magari yote ya Toyota yanayotumika katika kukabiliana na COVID-19 kwa muda ya siku saba bure, Familia ya Karimjee imetoa jenereta la KVA 180 lenye thamani ya sh. milioni 75.
Wengine ni Watoa
Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) ambao wametoa bidhaa mbalimbali
zikiwemo magari ya matangazo yatakayotumika kutoa elimu kwa muda wa miezi minne
kupitia kampuni ya Advent Construction, maji ya kunywa (Bakhressa Group),
Billboard (Ashton Media) vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh. milioni 150.
Shirikisho la Wenye
Viwanda Tanzania (CTI) walitoa matanki 1,000 yenye thamani ya sh. milioni 25,
huku kila moja likiwa na ujazo wa lita 250, matanki hayo yametengenezwa maalumu
kwa ajili ya kunawia mikono, pia Kampuni ya GS1 Tanzania Limited imetoa vitakasa
mikono chupa 1,600 zenye thamani ya sh. milioni nne.
Kadhalika, Tanzania
Oxygen ltd imetoa msaada wa sh. milioni 158 ambapo wamehaidi kufanyia ukarabati
kiwanda kikubwa cha kuzalisha oxygen, Mount Meru imetoa vitakasa mikono vyenye
thamani ya sh. milioni mbili, Hospitali ya Aga Khan imetoa dawa, sabuni, vitakasa
mikono na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 10.220.
Pia, kampuni ya gesi
ya Oryx imehaidi kutoa msaada wa kusambaza gesi kwa ajili ya kupikia na
matumizi mengine katika hospitali kama kufulia na kwenye vituo vya kuwahifadhi
watu wanaohisiwa kuwa pamoja wagonjwa wa COVID-19. Gesi hiyo ina thamani ya sh.
milioni 25, Tredea Cosmetics Ltd wametoa vitakasa mikono vyenye thamani ya sh. milioni 1.6.
Umoja wa Mama lishe-Ilala
na Machinga wa Kariakoo wametoa sabuni
na vitakasa mikono vyenye thamani ya sh. milioni mbili. Wakati huohuo, Chemba
ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) wametoa shuka 50,
magodoro10, sabuni za maji chupa 170 na vitakasa mikono chupa 400 vyote vikiwa
na thamani ya sh milioni tano.
Baada ya kupokea misaada
hiyo, Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli aliwashukuru wadau hao kwa
vitu mbalimbali walivyovitoa kwa ajili ya kupambana na COVID-19 kwani vifaa
pamoja na fedha walizozitoa zitaisadia Serikali katika kukabiliana na ugonjwa
huo.
Hata hivyo, Waziri
Mkuu alisema Serikali kwa upande wake inaendelea kuchukua hatua mbalimbali
katika kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hausambai zaidi
nchini. Alitumia fursa hiyo kuwashukuru madaktari, wauguzi pamoja na wataalamu
wengine kwa huduma wanazozitoa.
Kuhusu wadau wengine
wanaohitaji kutoa misaada, Waziri Mkuu amesema Ofisi yake iko wazi pia wanaweza
kupeleka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa
wanalio nje ya nchi au sehemu yoyote wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti yenye Jina la: National Relief Fund Electronic Akaunti Na: 9921159801
No comments:
Post a Comment