Na Mwandishi Wetu
IDARA ya Habari Maelezo, Zanzibar imesitisha mikutano ya waandishi wa habari na badala yake taarifa kuhusu corona zitatolewa mbashara kupitia Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Mkurugenzi wa idara hiyo, Dk. Juma Mohamed Salum aliyasema hayo jana katika taarifa yake kwenda kwa vyombo vya habari kuhusu maambukizi ya virusi vya corona.
Alisema katika kujikinga na maambukizi hayo ikiwamo kuepuka mikusanyiko, kuanzia Aprili 13 mwaka huu na kwamba taarifa zitaandaliwa kwa maandishi yaani ‘press release’.
“Taarifa kuhusu virusi vya corona zitatolewa kwa njia ya ‘press release’, kurusha matangazo moja kwa moja kupitia ZBC au kurekodiwa na kusambaza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari na umma kwa ujumla,” alisema Dk. Salum
katika taarifa yake.
Alieleza kuwa taasisi zote zenye shughuli zitakazojumuisha waandishi zitatumia njia zilizoelekezwa ili kujiepusha na corona.
“Wahariri na waandishi wa habari tunawasisitiza kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya na serikali kwa ujumla kwa kuepuka mikusanyiko,” alisema Dk. Salum.
No comments:
Post a Comment