Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona nchini. (Picha na Maktaba).
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
IDADI ya wagonjwa wa COVID-19 nchini, imefikia 46 baada ya leo kuongezeka wagonjwa 14.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliyasema hayo kupitia taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona nchini.
Alisema wagonjwa wapya 14 ni Watanzania na kati yao 13 ni wakazi wa Dar es Salaam na mmoja anatokea Arusha.
“Wizara inatoa taarifa ya ongezeko la wagonjwa 14 wa COVID-19 hadi kufikia 46 kutoka 32 tuliowatolea taarifa ya awali Aprili 10 mwaka huu,” alisema Ummy.
Taarifa hiyo ya Waziri Ummy ilisema wagonjwa wote wanaendelea vizuri na matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya na ufuatiliaji wa watu waliokuwa
karibu na wagonjwa hao unaendelea.
“Kwa mara nyingine serikali inarudia tena kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kama tunavyowapatia taarifa na elimu mara kwa mara kupitia njia mbalimbali za kujikinga hususan kuepuka misongamano na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima,” alisema
Waziri Ummy.
No comments:
Post a Comment