Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda
akizungumza wakati wa kikao kazi cha makatibu Wakuu na Wataalam wa Ubunifu na
Usanifu wa majengo leo Aprili, 20, 2020, lengo ikiwa ni kujadili mpango kabambe wa
Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba
Dodoma, Kikao kimefanyika katika Ukimbi wa Mkutano wa ofisi yake Dodoma, wa
kwanza kushoto ni Katibu wa kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia
Dodoma Bw. Meshack Bandawe.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la
Mji
wa Serikali Mtumba Dodoma, wakifuatilia kikao
hicho leo tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya
Waziri Mkuu, Dodoma, kulia ni,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano) Dkt. Jim Yonazi na (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo , Dkt. Hassan Abbas (katikati).
Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi
wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20,
Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri
Mkuu, Dodoma.
Na Mwwandishi Wetu
Ofisi ya Waziri Mkuu
inaendelea na zoezi la kuratibu awamu ya pili ya uendelezaji wa mji wa serikali
eneo la Mtumba, makao makuu ya nchi jijini Dodoma. Awamu hii ya pili inahusisha
Ubunifu na ujenzi wa majengo makubwa ya Ofisi zitakazotumiwa na Wizara za
serikali.
Akiongea, leo tarehe
20 Aprili, 2020, katika kikao cha Kamati
ya Makatibu wakuu na Wataalamu wa michoro ya Ubunifu na usanifu , Katibu Mkuu
ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge), Tixon Nzunda, amefafanua kuwa
awamu hii ya pili ya mpango huo inajikita katika kuboresha ubunifu na usanifu
wa mji wa serikali, ulioko Mtumba, Jijini Dodoma.
Aidha, kufanikiwa kwa mpango huo ni kutachangiza jiji la Dodoma kuwa jiji bora na la kisasa
linaloendana na mahitaji na mifumo ya majiji bora duniani. Ili kufikia azma
hiyo, tayari Timu ya Wataalam imepitia michoro
ya ubunifu na usanifu. Pia Wakala wa majengo Tanzania (TBA), inaendelea kufanya
kazi kwa karibu na Taasisi nyingine
zinazohusika na miundo mbinu katika mji wa Serikali kama vile TARURA, DOWASA,
TANESCO, ZIMAMOTO, TPDC, TTCL na eGA.
Hivi karibuni , Mwezi Februari mwaka huu, 2020,
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alizindua Mpango Kabambe wa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ambapo aliwataka wadau mbalimbali kutoa
ushirikiano kwa kiwango cha juu katika utekelezaji wa Mpango Kabambe wa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kulifanya kuwa jiji bora na la
kisasa nchini.
Serikali, kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kutekeleza zoezi la kuhamishia shughuli za
Serikali Kuu Dodoma. Tangu utekelezaji wa zoezi hilo uanze mwezi Septemba 2016.
Uamuzi wa kuhamishia
shughuli za Serikali Dodoma ulifanyika mwaka 1973 ikiwa ni maelekezo ya Chama
cha TANU kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa
awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
No comments:
Post a Comment