HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 28, 2020

PALESTINA YATOA MSAADA WA MASHINE YA MAJI TIBA KWA TANZANIA

 Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour AbuAli, akipita katika machine ya kusafisha mwili ‘Sanitization Machine’ iliyotolewa na ubalozi huo kama msaada kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona (COVID-19). (Na Mpiga Picha Wetu).

Serikali ya Palestina imetoa msaada wa mashine ya maji tiba, yaani sanitization machine kwa serikali ya Tanzania.

Katika azma ya kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kukabili changamoto ya kihistoria iliyoletwa na janga la COVID-19; serikali ya Palestina imetoa zawadi ya machine ya maji tiba (sanitization machine) kwa serikali ya Tanzania yenye uwezo wa kusafisha mwili mzima wa mtu.

Mashine hii imetengenezwa hapa hapa nchini kwa ushirikiano kati ya Mhandisi wa Palestina na wataalamu wa Tanzania.

akizungumza na waandishi wa habari Aprili 28, 2020, Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour AbuAli, amesema kwamba kupitia utamaduni wa kunawa na maji tiba ili kupunguza kuenea kwa COVID-19, serikali ya palestina imefanikiwa kuweka machine izi katika maeneo mbalimbali nyeti nchini mwao na kuona mafanikio na hivyo basi kuona umuhimu wa kuungana na Tanzania katika swala hili. 

Balozi amesema pia mashine hii ni rahisi kutumia na haina madhara yoyote kwa mtumiaji. Kwa kutumia mashine hii serikali ya Tanzania inajihakikishia kwa asilimia kubwa kupunguza ueneaji wa virusi vya corona (COVID-19), balozi pia amebaini kuwa juhudi hii ya serikali ya Palestina ni hatua ya kuimarisha ushirikiano baina ya Palestina na Tanzania katika kulinda wananchi wake dhidi ya janga la Corona ambalo kwasasa limedai vifo zaidi ya watu laki mbili.

Balozi pia alibaini kwamba ingawa palestina ina rasilimali chache, imedhamiria kuungana na serikali ya Tanzania kupambana vita vya Covid-19

No comments:

Post a Comment

Pages