Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini Arifu
Abri akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi msaada
uliopokelewa na mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.( Picha na
Denis Mlowe).
Na Denis Mlowe, Iringa
MJUMBE
wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini Arifu Abri
ametoa msaada wa chakula tani tatu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wa kijiji cha
Isele kilichoko tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa vijijini mkoanbi
Iringa kwa kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya chakula.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela,
Arifu Abri alisema kuwa changamoto
wanayokabiliana nayo wananchi wa kijiji hicho imepelekea kujitoa kuwasaidia
watu wenye mahitaji muhimu ili kuokoa maisha yao madhara waliyopata kutokana na
mafuriko hayo.
Alisema
alipata taarifa ya wananchi wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele kuwa
wamepatwa na mafuriko kutokana na kunyesha kwa mvua nyingi msimu huu wa kilimo
na kusabaisha hasara kubwa kwa wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo
lililotokea mafuriko na kutegemea zaidi kilimo kwa ajili ya maisha.
Alisema
kuwa moja ya mahitaji ambayo wahanga wa mafuriko wa kitongoji cha Mbingama ni
wananchi asilimia kubwa kukosa chakula cha kila siku hivyo ndio maana msaada
wangu nimejielekeza kwenye kutoa chakula zaidi ambapo utawasaidia kwa kipindi
hiki cha mafuriko.
“Najua
kuna wadau wengine wameshatoa baadhi ya msaada kulingana na mahitaji hata hivyo
kwa upande wangu mimi nimeamua kutoa chakula kulingana na mahitaji ambayo
nimeona wanahitaji wahanga wa mafuriko wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha
Isele Tarafa ya Pawaga” alisema
Abri
alitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza kuwasaidia wahanga hao wa
mafuriko katika kitongoji cha Mbingama ili kuwasaidia kurudi kwenye maisha
ambayo walikuwa wameyazoe hapo awali kulingana na shughuli ambazo walikuwa wanazifanya
kupa riziki zao.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela mara baada ya kupokea
msaada huo alimshukuru mjumbe wa mkutano mkuu ccm taifaArifu kwa msaada huo kwa
kuwa umekuja katika wakati mwafaka kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo
wananchi hao.
Aidha
Kasesela alitoa wito kwa wadau kujitokeza zaidi kuwasaidia wananchi hao ambao
licha ya changamoto ya chakula wanakabiliwa na changamoto ya nguo, makazi,
madawa kwa lengo la kuweza kuondokana na hali hiyo.
No comments:
Post a Comment