Mfanyakazi wa Kituo cha Mafuta cha Puma kilichoko mtaa wa Jamhuri
jijini Dar es salam akipulizia dawa baadhi ya magari yanayofika kituoni
hapo kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona. (Picha na Denis Mlowe).
Na Denis Mlowe
KATIKA harakati za
kupambana na virusi vya Corona nchini, kituo cha Mafuta cha Puma UMMA Mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam wameanzisha utaratibu wa kupuliza dawa za kuua
vijidudu kwa wateja wote wanaokwenda kujaza mafuta katika kituo hicho.
Akizungumza
na Habari Mseto Blog, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mohamed Ally, alisema kuwa utaratibu wa kupuliza
dawa magari yanayofika katika vituo hivyo vya Mafuta kila siku.
Alisema
mlipuko wa virusi vya corona ukiendelea kuathiri sekta zote duniani,
mataifa mengi yameshindwa kupata jibu la kukabiliana na janga hivyo
hakuna budi kuanza kupambana mapema visiendelee kuenea kwa kasi nchini.
Alipounga
mkono kitendo cha agizo la kufungwa kwa shule na vyuo vyote nchini
kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.
Aidha
alipongeza kitendo Cha serikali kuarisha maadhimisho ya Sherehe za
Muungano, tarehe 26 Aprili 2020 pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi, Mei
Mosi, 2020 ili kuepuka msongamano wa watu.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa kitendo Cha Rais John Magufuli kusema
watu wafunge na kusali ni jambo muhimu sana kwa sasa kwani kimbilio la
kweli ni MUNGU.
No comments:
Post a Comment