Mkuu wa shule ya Kihangaiko Kanali Sijaona Myala katikati akishangilia na Kuruti mara baada ya kumaliza zoezi la Mwisho kwa Kuruti hao katika pori la Msata bagamoyo Mkoani Pwani. ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Baadhi ya askari na wanafunzi Kuruta wa Shule ya Aawali ya Mafunzo
ya Kijeshi RTS Kihangaiko wakishangilia juu ya kifaru baada ya kumaliza zoezi Maliza Msata Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali
Alfred Kapinga amewataka Askari wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ
kuendelea kufanya kazi mama ya Ulinzi wa mipaka na raia kwa nguvu zote.
Meja Jenerali Kapinga alisema hayo wakati akihitimisha mafunzo ya porini kwa kuruti
kutoka shule ya mafunzo ya awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko kundi la 39
yaliyofanyika kwa siku 14 katika Pori la Pongwe Msungura Bagamoyo Mkoani Pwani.
Meja Jenerali Kapinga aliwataka kuruti hao kujiandaa kufanya
kazi ya Ulinzi wa raia kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanatimiza jukumu la
Msingi litakayoijenga Nchi yetu na kuifanya kukua kiuchumi.
“ Kazi mama ya Jeshi letu ni kulinda mipaka ya nchi na
kuwalinda Raia wa Nchi yetu ili waweze kushiriki shughuli za uzalishaji mali kwa
Amani na kuletea Taifa Tija inayokusudiwa na kazi hiyo hufanywa na watu imara ambao ni wanajeshi” Alisema Meja Jenerali Kapinga.
Meja
Jenerali
Kapinga amewasihi kuruti kuendelea kuweka juhudi kwani jeshi lipo imara
siku zote na linahitaji watu imara katika kutekeleza majukumu ya
kuilinda nchi hivyo mbali na mazoezi walinde Afya zao dhidi ya magonjwa
kama Corona na Ukimwi.
Aidha aliwataka wakuu wa Vikosi Jirani na maeneo ya
mazoezi kuyadhibiti maeneo hayo kwa namna yeyote yasivamiwe na na Wananchi kwani maeneo hayo ni muhimu kwa
ustawi wa jeshi.
“ Hakuna sababu
kwa Pori kama hili la Pongwe Msungura Msata kuwaachia raia kwani tumeshawaachia
maeneo mengi na katika eneo hili yapo maeneo mengi hakuna sababu ya wao kuingia
katika eneo letu la mazoezi ” Alisema Meja Jenerali Kapinga.
Aliongeza
kuwa eneo hilo licha ya kuwa halijavamiwa kwa ujenzi lakini wafugaji na
wakataji wa miti wachache wameanza
kuingia bila kujali kuwa eneo hilo limekuwa likitumika tangu kipindi cha
Wagombea Uhuru kwa mazoezi ya Kijeshi.
Aidha amewataka kufanya mazoezi ya mara kwa mara
kuepusha Wananchi kuyavamia wakidhani hayana matumizi kwani wakipoteza maeneo
hayo hakutakuwa na maeneo mengine.
Aidha alitoa wito kwa raia kutoingia hovyo katika
maeneo ya mazoezi ya Kijeshi kwani wanaweza kupatwa na madhara mbalimbali
ikiwemo ulipukiwaji wa Mabomu na madahara mengine.
Awali akimkaribisha Mkuu wa shule ya Kihangaiko
Kanali Sijaona Myala amesema mafunzo hayo ni moja ya mafunzo ya msingi ya kuwaimarishaAskari
katika maisha yao wakiwa jeshini.
Alisema walihakikisha wanajumuisha Vikosi mbali mbali
ambavyo humsaidia Askari akiwa Vitani ili kuendelea kuhakikisha tunakuwa na
Askari bora wenye Viwango ambao mara zote wamekuwa wakililetea sifa jeshi na
Nchi kwa Ujumla.
Pia aliwataka kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya
Ugonjwa wa Corona kwani hakuna adui mdogo na kwa kufanya hivyo kutawabakisha
salama na kuitumikia nchi kikamilifu.
Baadhi ya Askari kuruti Diana Gamanywa na Emanuel
Maganga kwa nyakati tofauti wamesema wamejifunza vitu vingi ambavyo
vimewaimarisha hasa katika medani ya Vita na kusaidia mamlaka za Kiaraia katika
majanga mbalimbali
Katika mazoezi hayo vifaa vya kivita vikiwemo,
Ndege, Vifaru,Mizinga na ulipuaji mabomu, pamoja na bunduki za askari vilitumika
katika kuonyesha uwezo wao wa mapambano dhidi ya Adui.
No comments:
Post a Comment