HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 17, 2020

Kabati ateswa unyanyapaa wa walemavu

 Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati, akikabidhi vitakasa mikono kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona.
 Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati, akikabidhi vitakasa mikono kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona.
 Vitakasa mikono vilivyokabidhiwa,
 Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati, akikabidhi barakoa kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona.
 Picha ya pamoja.


NA MWANDISHI WETU

JAMII mkoani Iringa imetakiwa  kushirikiana na kutowanyanyapaa watu wenye ulemavu  hasa katika kipindi hiki ambacho kuna mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa  wa COVID-19.

Rai hiyo imetolewa jana na Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati wakati akitoa msaada wa vifaa vya kujikinga na corona kwa walemavu wa mkoa huo.

Mbunge huyo alisema kila mtu ni mlemavu mtarajiwa hivyo hakuna sababu ya kuwanyanyapaa na kuahudi kuendelea kuwa karibu na kundi hilo na atashirikiana nao kwa kila hatua.
 
Kabati amempongeza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana na wenye Ulemavu,  Stella Ikupa kwa namna anavyojitolea kwa watu wenye ulemavu nchini jambo ambalo linawapa moyo walemavu wote.

Katika hatua nyingine Kabati amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya watu wenye ulemavu.

"Naomba jamii ijiepushe na tabia ya kunyanyapaa watu wenye ulemavu wana haki sawa na wasio na ulemavu lakini pia kila mtu ni mlemavu kiasili," alisema.

Mwenyekiti  wa Walemavu Mkoani Iringa Shabani Shomari amemshukuru Mheshimiwa  Kabati kwa kutoa vifaa hivyo na kusema kundi hilo limekuwa likitengwa na kusahaulika  katika kupewa misaada  kama hiyo.

Alisema walikuwa na uhitaji wa vifaa hivyo ili waweze kuwa katika mazingira salama kipindi hiki cha COVID-19.

Nao baadhi ya walemavu  wamemshuru Mheshimiwa Kabati kwa kuapa vifaa hivo ambavyo vimetengenezwa kwa mazingira rafiki kwao kwani wakati mwingine wanakumbana na vifaa ambavyo sio rafiki na kujikuta wanashindwa kunawa na ikizingatiwa maambukizi yanaongezeka.

No comments:

Post a Comment

Pages