Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.
Innocent Bashungwa na Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiendesha Kikao kilichowakutanisha wamiliki wa
viwanda vya vifaa kinga kwa lengo
kujadili upatikanaji na uzalishaji wa vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na
Corona. Leo 13.05.2020 jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa Pamoja na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,
Mh. Ummy Mwalimu wameendesha Kikao cha Wadau kujadili upatikanaji na uzalishaji
wa vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na COVID – 19 leo tarehe 13.05.2020
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent
Bashungwa amewapongeza wamiliki wa viwanda hivyo kwa kubuni na kugundua
teknolojia na uzalishaji wa vifaa kinga
kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.
“Kuanzisha viwanda ni sehemu ya ulinzi wa nchi,hivyo kuwa na
viwanda vyetu nchini hususani wakati wa shida imesaidia upatikanaji wa baadhi
za vifaa kinga kwa bei nafuu”.Alisema
Waziri Bashungwa
Waziri Bashungwa ameitaka MSD kununua vifaa kinga vinavyozalishwa na
viwanda vya ndani ambavyo vimekidhi viwango na vimesajiliwa na TMDA badala ya
kutumia fedha iliyotengwa na Serikali kununua vifaa hivyo nje ya nchi.
Waziri Bashungwa ameahidi kukitembelea
kiwanda cha Msagala Investment kilichopo Bagamoyo ambacho kinatarajia kuanza
kuzalisha malighafi za utengenezaji wa barakoa kutokana na pamba zinazolimwa
nchini.
Amesema katika kikao hicho wamekubalia
kujipanga vizuri katika uzalishaji wa vifaa kinga na hivyo wamewataka Shirika
la Maendeleo la Taifa (NDC) kujikita katika kuzalisha barakoa aina ya N95 na
glove kutokana na kwamba viwanda vya namna hii havipo nchini.
Pia Waziri Bashungwa ameitaka TMDA
kushirikia na wizara ya viwanda kuisaidia NDC kuweza kufanya kiwanda hicho kuanza kuzalisha kwa
wakati na hivyo kusaidia watumishi wa afya walio mstari wa mbele kutoa huduma
bila hofu.
Kwa upande wa MSD, Waziri Bashungwa
ameitaka kununua vifaa kinga
vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ambavyo vimekidhi viwango na vimesajiliwa
na TMDA badala ya kutumia fedha iliyotengwa na Serikali kununua vifaa hivyo nje
ya nchi.
Waziri Bashungwa ameahidi kukitembelea
kiwanda cha Msagala Investment kilichopo Bagamoyo ambacho kinatarajia kuanza
kuzalisha malighafi za utengenezaji wa barakoa kutokana na pamba zinazolimwa
nchini.
Katika
kuchukua hatua zaidi, Waziri Bashungwa amewasihi wazalishaji wa vifaa tiba
kuongeza jitihada za kuzalisha ili kuendana na kasi ya soko Pamoja na
kuhakikisha Watanzania wanakuwa salama kipindi hiki cha COVID-19
Pia
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli
kwa kuhimiza sera ya Tanzania ya Viwanda kwani sera hiyo imekuwa ya manufaa sana
hasa kipindi hiki cha COVID-19 kwani vifaa vingi vinazalishwa hapa ndani bila
kutegemea kuagiza kutoka nje ya nchi.
“Rais aliona mbali, kuwa na viwanda vyetu hapa
nchini hata wakati wa shida, viwanda hivi vingekuwa havipo tungepata shida
sana,”Amesema Bashungwa.
Katika
hatua nyingine, Waziri Bashungwa amempongeza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa
hatua Madhubuti anazozifanya katika kukabiliana na COVID-19
“Nakupongeza
sana kwa kusimamia Wizara ya Afya, tunakushukuru kwa umahiri wako, taifa hili
tunakutegemea,” amesema Bashungwa.
Aidha, Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda
vya dawa na vifaa tiba kuzalisha vifaa kinga vya kutosha ili kukabiliana na
janga la Corona nchini ili kuondokana na changamoto ya ucheleweshaji wa kupata
vifaa kinga kutoka nje ya nchi
“Tukizalisha hapa nchini tutaokoa rasiliamali fedha nyingi,
muda pia tutazalisha ajira na kuwa na uhakika wa ubora na usalama unaohitajika kupitia
mamlaka zetu za ndani kwa urahisi”.
Alisema Waziri Ummy.
Waziri amesema kuwa bado kuna uhitaji
mkubwa wa vifaa kinga , hivyo wale wote wanaozalisha vifaa kinga wanatakiwa
kuongeza uzalishaji ili kutosheleza mahitaji ya soko nchini na hata kuweza
kuuza nchi za jirani.
No comments:
Post a Comment