Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ( NEC), lililopo Njedengwa, jijini Dodoma, linalojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT, May 5, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa
na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) linalojengwa
na Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma.
Novemba 18, 2019, Waziri Mkuu alitembelea
mradi huo na kuonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa mkandarasi aliyekuwa
akijenga jengo hilo ambaye ni Wakala Majengo Tanzania (TBA) na kuagiza kuvunjwa
kwa mkataba.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Mei
13, 2020) wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la NEC.
Amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa na anaamini litakamilika kwa wakati.
“…Ninahakika mkiongeza nguvu katika baadhi ya
maeneo tutafika na haya ndio Serikali inataka kuona taasisi zake zikifanya.
Kwenye jengo hili ndipo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa
kuchukua fomu.”
Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo
kuipongeza Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT kwa namna walivyoratibu vizuri ujenzi
wa jengo hilo. “Miradi mingi waliyokabidhiwa Suma JKT imekuwa ikijengwa kwa
weledi mkubwa.”
Kwa
upande wake,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenyeulemavu,
Jenista Mhagama amesema Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT ilikabidhiwa mradi wa
ukamilishaji wa jengo hilo Desemba 24, 2019 na unatarajiwa kukamilika Mei 30,
2020.
Amesema mradi huo unaosimamiwa na Chuo Kikuu
Ardhi (ARU) kama mshauri wa mradi hadi leo (Mei
13, 2020) ujenzi wa jengo kuu la ofisi umefikia asilimia 85, jengo la
kutangazia matokeo ujenzi wake umefikia asilimia 68, kazi za nje zimefikia
asilimia 85 huku jengo la ghala limefikia asilimia 92.
Naye, Mkurugenzi wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amesema mkataba wa mradi huo ulipaswa
ukamilike Aprili 30, 2020 lakini baada ya kutembelea eneo la mradi
wamekubaliana kuwa kazi hiyo iwe imekamilika ifikapo Mei 30, 2020 na Juni 1,
2020 watumishi wahamie na kuanza kazi.
Amesema mradi huo unagharimu zaidi ya sh.
bilioni 12 na tayari zaidi ya sh bilioni sita zimeshatolewa na kwamba kazi
zinazoendelea kwa upande wa jengo kuu la ofisi ni pamoja na kupachika milango
na madirisha, kupaka rangi na kuweka vigae kwenye sakafu.
No comments:
Post a Comment