Mwenyekiti wa JOWUTA, Claud Gwandu. |
Na Mwandishi Wetu
CHAMA
cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimesisitiza
umuhimu wa waandishi wa habari nchini kuendelea kuzingatia maadili,
kanuni na sheria katika utekelezaji wa majukumu yao katika kipindi hiki
cha mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu COVID19.
Akitoa
salamu za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari Duniani leo,
Mwenyekiti wa JOWUTA, Claud Gwandu, alisema uhuru wa habari, maadili,
haki, usawa ni nguzo muhimu za kuzingatiwa na wanahabari nchini katika
kipindi hiki kigumu ambapo dunia nzima inapambana na COVID-19.
"Tunapotekeleza
majukumu yetu muhimu ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha,
tunapaswa kuchukua tahadhari zote za kiusalama kwa kuepuka mikusanyiko
isiyo ya lazima, kuvaa vifaa kinga kama barakoa na kufuata maelekezo ya
wataalam wa afya ili kuepuka kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Alisema
JOWUTA inaunga mkono kauli mbiu ya Siku ya Uhuru wa Habari 2020 ambayo
inasitiza waandishi kufanya kazi bila hofu ua upendeleo ili kuonesha
umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari hasa kipindi hiki cha maambukizi
ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
Gwandu
aliwataka waandishi kuadhimisha siku hii kwa kukumbushana kusimamia
maadili ya uandishi wa habari kwa kuwa wao ni kioo cha jamii.
"Tunaadhimisha
siku ya uhuru wetu huku duniani ikipitia wakati mgumu wa mapambano
dhidi ya COVID-19 ni imani yangu kuwa tutasimamia maadili, uadilifu,
haki, usawa, kanuni na sheria zinazosimamia taaluma yetu," alisema.
Mwenyekiyi
huyo alisema iwapo kundi hili litakuwa na mshikamano na ushirikiano na
wadau wa maendeleo na serikali malengo ya kuifikisha Tanzania ya viwanda
na uchumi wa kati itafanikiwa.
"Nasisitiza
umuhimu wetu kwenye jamii asitokee kati yetu anakubali kutumika kwa
maslahi ya mtu binafsi.Tambua utakuwa umesaliti Watanzania zaidi ya
milioni 50," alisema.
Gwandu
alitumia siku hiyo kuwahamasisha waandishi wa habari nchini kujiunga na
JOWUTA ili kwa pamoja waweze kupigania haki zao za msingi.
Alisema
jukwaa pekee ambalo waandishi nchini wanaweza kufikisha malalamiko na
changamoto zao ni JOWUTA hivyo hawanabudi kujiunga kwa sasa.
No comments:
Post a Comment