Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela, akizungumza katika kikao cha Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje la kujadili hoja za Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo amewataka watumishi waliotumia
fedha za Serikali wazirudishe.
Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wakiwa katika Baraza la Madiwani la kujadili hoja
za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo Mkuu wa Mkoa wa
Songwe amewataka watumishi waliotumia fedha za Serikali wazirudishe.
Na Mwandishi Wetu
Watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje walio tumia fedha za makusanyo ya ndani kiasi
cha shilingi milioni 22.083 wametakiwa kuzirudisha ndani ya siku tatu huku Taasisi
ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU ikielekezwa kusimamia hilo.
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ametoa agizo hilo jana wakati wa kikao cha
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG).
Brig. Jen, Mwangela
amesema hakuna mtumishi au mtu yeyote atakayetumia fedha za Serikali kwa Mkoa
wa Songwe akabaki salama hivyo wote wanaodaiwa kukusanya mapato ya ndani na
kuyatumia waziridishe au wakamatwe hadi watakapo zirudisha fedha hizo.
Amesema TAKUKURU
hawapaswi kucheka na wala fedha za serikali kwakuwa madiwani wanahangaika kwa
kushirikiana na serikali kubuni vyanzo vya mapato ili fedha hizo zitakazo
kusanywa ziboreshe huduma za jamii na kukuza uchumi hvyo wanaozitumia hawapaswi
kuvumiliwa.
Brig. Jen Mwangela
ameongeza kuwa katika taarifa ya CAG Halmashauri ya Wilaya Ileje imepata hati
yenye mashaka katika kuzingatia taratibu na sheria za manunuzi hivyo Mkurugenzi
ahakikishe wataalamu wake wanafuata sheria na taratibu za Manunuzi pia madiwani
wahahakishe wana simamia watumishi wasikiuke taratibu hizo.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Haji Mnasi amemshukuru Mkuu
Wa Mkoa wa Songwe kwa kushiriki kikao hicho na kuahidi kuwasimamia watumishi
wafuate taratibu na sheria.
No comments:
Post a Comment