Ofisa
usafirishaji wa Kampuni ya Usafirishaji (ATT) Godfrey Tarimo(kushoto) akikabidhi jana msaada ya
barakoa ya thamani ya milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia). (Picha na Tiganya Vincent).
Na Tiganya Vincent
KAMPUNI ya Usafirishaji
ya Athwal (ATT) ya mjini Tabora imetoa msaada wa barakoo zenye thamani ya
shilingi milioni 20 kwa uongozi wa Mkoa
wa Tabora.
Msaada huo umekabidhiwa
jana na Ofisa usafirishaji wa ATT Godfrey Tarimo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili
kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.
Alisema Kampuni hiyo
ambayo inatoa huduma za usafirishaji ndani na nje ya Tabora imeamua kutoa msaada
huo ili uweze kusaidia katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona
yanayoendelea mkoani Tabora.
Akipokea msaada huo Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, alisema msaada huo umekuja wakati muhimu
ambapo Taifa liko katika vita ya kudhibiti ugonjwa wa Covid- 19 usiendelee
kusambaa.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema
wadau wote Mkoani humo wanapaswa kuungana katika vita ili hatimaye waweze
kuushinda ugonjwa wa Covid-19.
Alisema msaada huo walioupokea
baada ya kudhibitishwa na wataalamu wa sekta ya afya kuwa ziko vizuri zitagawanywa
katika Wilaya zote za Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuwasaidia watoa huduma za
afya ambao wanasaidia kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 na watu wengine ambao
hajiwezi.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa
wito kwa wadau wengine wanaoendesha shughuli zao ikiwemo za biashara kuendelea
kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya janga la Corona.
No comments:
Post a Comment