HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 03, 2020

MKUU WA MKOA WA TABORA AAGIZA KUFUNGWA VIPAZA SAUTI MAENEO YA SOKONI NA STENDI KUTOA ELIMU JUU YA CORONA

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati), akipokea msaada wa ndoo mbili zinazoruhusu mtu kunawa bila kushika kutoka kwa Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo-SIDO-Mkoani Tabora, Samwel Neligwa (mwenye T-shirt ya rangi ya chungwa). (Picha na Tiganya Vincent).


Tiganya Vincent

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza maeneo yote yanayotoa huduma kama vile sokoni na stendi kufungwa vipaza sauti ili watu wanaofanyika kazi maeneo hayo waendelea kupata elimu ya kujikinga na Covid -19.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha wasafiri na wafanyabiashara wanaokuwepo katika maeneo hayo wanapata elimu sahihi ya kukabiliana na kujikinga virusi vya Corona.

Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati alipokutana na viongozi wa masoko , Stendi na wajane wakati akiongoza timu ya wataalamu wa afya kutoa elimu ya kujikinga na covid -19.

Alisema kuwa kila siku Redio zilizopo mkoani Tabora kupitia uongozi wa Mkoa na wataalamu wamekuwa wakiendesha vipindi vya elimu ya kujikinga na virusi vya Corona kwa wakazi wa Tabora.

Mwanri aliutaka uongozi wa Manispaa ya Tabora na Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha wanafunga vipaza sauti katika maeneo ya biashara na kuendelea na matangazo ya magari mitaani ya kuwaelimisha wananchi kuchukua hatua za kujikinga na Virusi vinavyosababisha Covid-19.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora amewaagiza Watendaji wa Vijiji kuwatangazia wananchi katika maeneo yao kufungulia Redio zilizopo Mkoani humo ili waweze kupata elimu sahihi ya kukabiliana na virusi vya Covid -19.

Alisema Redio zilizopo mkoani Tabora kila siku zimekuwa zikitoa muda kwa watalaamu wa sekta ya afya kuelezea mikakati na mbinu mbalimbali ambazo wananchi wanatakiwa kuchukua ili kujilinda wasiweze kupata maambukizi ya Corona.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Mamlaka ya Maji safi Tabora (TUWASA) kuhakikisha maeneo ya shughuli nyingi kama vile sokoni na stendi kunakuwepo na maji ya kutosha wakati ili watu waweze kunawa mikono.

No comments:

Post a Comment

Pages