Na Tiganya Vincent
WATUMISHI wa umma wameonywa
kutotumia mitandao ya kijamii ambayo sio rasmi katika usambazaji wa nyaraka
mbalimbali za umma zikiwemo barua za kikazi katika Ofisi nyingine za umma.
Kauli hiyo imetolewa jana
na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dustan Shimbo wakati akitoa mada kwenye mafunzo
ya siku mbili ya awali kwa ajira mpya za Watendaji Kata, Watunza kumbukumbu,
Makatibu Mahsusi, Madereva na Maafisa Tehama
Alisema ni marufuku
kutumia barua za Kiserikali kwa kutumia mitandao kama ‘WhatsApp, facebook,
na e-mail’ binafsi kwa kuwa kufanya
hivyo ni kinyume na matakwa ya Sheria ya
Usalama wa Taifa ya mwaka 1970.
Shimbo alisema kuwa
Sheria hiyo imepiga marufuku wa utoaji wa nyaraka zote zilizohifadhiwa bila
kufuata taratibu unaotakiwa na kuongeza unaweza kupelekea nyaraka hizo kuzagaa
mitaani.
Alisema hatua hiyo
inaweza kupelekea jamii kupokea taarifa
ambazo sio rasmi na ambazo hazikuwafanyiwa utafiti na hazikutoka Mamlaka
inayopaswa kuzitoa , jambo ambali linaweza kupelekea kuzuka kwa taharuki katika jamii na
kuhatarisha usalama.
Shimbo alisema Mtumishi
ambaye hakupewa Mamlaka ya Utoaji wa Taarifa akifanya kosa hilo atafungwa kwa
kipindi cha miaka isiyozidi 20.
Alitoa wito kwa watumishi
kuendelea kuzingatia taratibu zinazoruhusiwa kisheria katika usambazaji wa
taarifa rasmi na kuachana na zile ambazo hazikubaliki ili kuwa na mazingira
salama katika uendaji kazi wao.
Mmoja wa Watumishi wapya
wa Halmashauri hiyo Scolastica Francis alisema kuna umuhimu sana kwa watumishi
wa umma kutunza siri kwa sababu unasaidia katika kuimarisha umoja ndani ya
utumishi wa umma.
Alisema utoaji wa siri
unaweza kusababisha baadhi ya watumishi kuvamiwa kama wanapokuwa wamepata
malipo yao stahiki.
No comments:
Post a Comment