Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Watendaji wa juu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar (kulia).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein kifafanua jambo kwa Ujumbe wa Watendaji wa juu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na Watendaji Wakuu Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu na Makamu Mwenyekiti Mohammed Khamis Hamad.
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed
Shein amesema kuwa Serikali inatekekeleza utawala bora kwa wananchi kwa
kuwapatia huduma za jamii zikiwemo elimu na afya zinazotolewa bure.
Akizungumza
alipokutana na ujumbe wa watendaji wa juu wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora Ikulu Zanzibar, Dkt. Shein alisema kuwa Serikali
inatakeleza kwa vitendo dhana ya utawala bora ikiwa ni utekelezaji wa
dhana iliyoasisiwa na Hayati. Abeid Aman Karume baada ya Mapinduzi ya
Mwaka 1964.
“Lengo
kuu la mapinduzi wakati huo lilikuwa ni kuhakikisha haki za binadamu
zinatekelezwa kwa kila mwananchi hapa Zanzibar, kwa hiyo Hayati. Abeid
Aman Karume aliiongoza Zanzibar kulete haki hizo ikiwemo elimu, afya na
ardhi ambapo kabla ya hapo huduma zilikuwa zinatolewa kwa madaraja, hasa
sekta ya afya na elimu daraja A lilikuwa la Waingereza, B lilikuwa la
zile familia za kisultani, C watu wa katikati na D watu wa kawaida ambao
kimsingi walikuwa wanapata huduma mbovu, kwa hiyo suala la utekelezaji
wa haki za binadamu lina historia kwa hapa Zanzibar”, alisema Dkt.Shein.
Alibainisha
kuwa baada ya Mapinduzi wananchi walianza kupata haki zao za msingi
ikiwemo elimu, kuanzia darasa la kwanza hadi la nne na kuanzia darasa la
tano kulikuwa na malipo ambayo yalimnyima mwananchi wa hali za chini
haki hiyo.
Kwa
upande wa ardhi, Dkt. Shein alisema kuwa ilikuwa ni ngumu kwa wananchi
wa Zanzibar kumiliki ardhi kabla ya mapinduzi kwani ardhi iligawiwa kwa
wageni na wenyeji kuwa wafanyakazi wa mashamba ya wageni, lakini baada
ya mapinduzi kila mwananchi alikuwa na uhuru na haki ya kutumia ardhi
kwa mujibu wa sheria.
Alifafanua
kuwa mambo hayo matatu ni ishara ya kwamba SMZ imeanza utekelezaji wa
Utawala bora na Haki za Binadamu mara tu baada ya kuidai haki hiyo kwa
wakoloni, na hii ilileta furaha kwa kila Mzanzibar kupata haki zake za
msingi kama vile ardhi, afya na elimu bure amabapo mpaka sasa Serikali
inatoa huduma hizo bure kwa asilimia 100.
Naye,
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu
Mathew Mwaimu amesema kuwa chini ya Uongozi wa Rais. Shein utawala bora
na utekelezaji wa haki za binadamu umeonekana wazi kwa kuwa hadi sasa
Serikali yake inatoa huduma za afya na elimu bure kwa kila mwananchi.
“Mhe.
Rais kutokana utekelezaji wa utawala bora na haki za
binadamu, Zanzibar imeendelea kuwa na amani, lakini pia wananchi
wameendelea kupata huduma za afya na elimu bure, hii ndiyo dhana ya
utawala bora”, Jaji Mwaimu.
Alibainisha
lengo la kumtembelea kuwa ni kuweka ukaribu na Serikali yake ikiwa ni
pamoja na kutekeleza majukumu ya tume hiyo ambayo ni kufuatilia
utekelezaji wa haki za msingi za wananchi.
Aidha,
Jaji Mwaimu aliipongeza SMZ kwa kushughulikia vizuri janga la ugonjwa
wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona,
kwani Serikali hiyo ilikuwa bega kwa bega na wananchi kwa kuwapa moyo
wa kufanya kazi huku wajikinga na maradhi hayo na mpaka sasa janga hilo
limepungua kwa kiasi kikubwa.
“Serikali
imechukua hatua kubwa kushughulikia janga la corona na tunashukuru
kwamba viongozi wote wa pande zote mbili mmekuwa na busara kubwa kwenye
mapambano hayo pamoja na maagizo yaliyokuwa yanatolewa na Shirika la
Afya Duniani (WHO) ikiwemo kufungia watu ndani, lakini nyinyi mlisema
watu wafanye kazi na sasa tumeshinda”, Jaji Mwaimu.
No comments:
Post a Comment