Diwani wa Mwangata Nguvu Chengula, akizungumza na wanahabari. (Picha na Denis Mlowe).
Na Denis Mlowe, Iringa
DIWANI
wa Kata ya Mwangata iliyoko Manispaa ya Iringa,Nguvu Chengula ameapa
kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Rais John Pombe Magufuri
anashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa 2020 unaotarajiwa
kufanyika Oktoba.
Akizungumza
na wanahabari kwenye ukumbi wa Boma, Chengula alisema kuwa atatumia
jitihada zote pamoja na Mali anazomiliki kuhakikisha CCM inashinda chini
ya Rais Magufuli kwa kutoa magari ya kampeni na vipaza sauti katika
kuhakikisha anarudi madarakani.
Alisema
kuwa kazi ambazo zimekwisha fanywa na Rais hadi sasa zimemfanya
atangaze Rais Magufuli ndio mtu pekee ambaye anafata nyendo zake katika
suala zima la uongozi.
Chengula
ambaye ni mmiliki wa shule za Sun Academy zilizoko Manispaa ya Iringa
alisema kuwa tangu rais Magufuli aingie madarakani amefinikisha mambo
mengi ikiwemo vijiji 3559 kupata umeme Jambo ambalo lilikuwa ni ndoto na
vijiji 4314 vinaendelea kupata nishati hiyo katika awamu ya pili.
Alisema
Rais Magufuli kwa kipindi Cha miaka 5 amefanikiwa kufanikisha ujenzi wa
vituo vya afya na zahanati zaidi ya 1000 hospitali 25 kitu ambacho
kilishilindikana katika awamu nyingine.
Aliongeza
kuwa katika suala la maji zaidi ya miradi 1571 imekamilika na vituo vya
maji 126610 vimejengwa na kuweza kuhudumia watu milioni 31.65 kwa ajili
ya watu wa vijijini.
Aliendelea
kumsifu Rais Magufuli kwa kuwezesha wananchi wanaendelea kunufaika na
mikopi isiyo na riba toka halmashauri zote nchini Jambo lililopewa
msukumo mkubwa na na kuhakikisha kwamba tozo za mazao zimeondolewa hivyo
kuwapa nafasi wakulima kuinua vipato vyao.
Akizungumzia
miundo mbinu alisema kuwa serikali ya Magufuli imefanikiwa kuboresha
Barabara ambapo zimejengwa kwa asilimia 98 kuunganisha mikoa yote
nchini.
Aliongeza
kuwa katika suala la elimu serikali imefanikisha kutolewa kwa bilioni
24.4 kila mwezi kwa shule za sekondari na msingi na kuongeza shule za
msingi kutoka 16,899 mwaka 2015 Hadi 17,804 mwaka 2020 na sekondari toka
4708 Hadi 5330 mwaka 2020.
Aidha
akizungumza kuhusu kata anayoongoza aliwashukuru wananchi kwa kumchagua
na kusema kuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhakikisha anatimiza
ahadi alizoahidi walipomchagua 2108.
Alisema
kuwa amehakikisha Barabara za kata hiyo zinapitika ili kurahisisha
shughuli za kiuchumi na kijamii kufanyika na kujenga Barabara ya lami
toka Zizi la Ng'ombe Hadi Ngelewala yenye km 1.4 kwa thamani ya sh.
Milioni 600,000,000.
Aidha
alifanikiwa kufanikisha uchimbaji wa mtaro wa maji mtaa wa Mwangata C
kwa gharama ya sh.milioni 3.5 aidha kujenga chumba Cha darasa kwenye
shule ya sekondari Mawelewele.
No comments:
Post a Comment