HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 16, 2020

ELIMU NI MUHIMU KUDHIBITI SUMUKUVU NCHINI

Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Wizara ya Kilimo Dkt .Honest Kessy (aliyevaa tai) akifungua mkutano wa wadau kujadili Mkakati wa Taifa wa Mawasilino Kudhibiti Sumukuvu uliofanyika Morogoro leo.Wa kwanza kushoto ni Clepin Josephat Mratibu wa TANIPAC na kulia wa kwanza ni Bw.Hamad Masoud Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Zanzibar na Dkt.Happy Magoha.
Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa chakula toka wizara ya Kilimo Dkt.Hones Kessy akifungua mkutano wa wadau kujadili rasimu ya Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano  Kudhibiti Sumukuvu uliofanyika chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mjini Morogoro leo.
Sehemu ya wadau walioshiriki mkutano wa kujadili Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano ili kudhibiti Sumukuvu mjini Morogoro leo. (Picha na Habari Wizara ya Kilimo).


 Na Mwandishi Maalumu

Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Kilimo wamekutana kupitia rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Mawasiliano ya kudhibiti sumukuvu ili kuwezesha jitihada za kukabililiana na tatizo hilo miongoni wananchi, hususan wakulima wa mazao.

Akizungumza kwenye mkutano huo, mjini Morogoro leo (16.06.2020) Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka Wizara ya Kilimo, Dkt. Honest Kessy alisema lengo la serikali ni kuhakikisha elimu juu ya tatizo la sumukuvu inatolewa kwa wakulima na wananchi kwa usahihi.
 
Alisema kuwa,mawasiliano yasipowekwa vizuri, yanaweza athiri wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo katika kumaliza tatizo la sumukuvu.

“ Mkutano huu unalenga kupokea maoni ya wadau wa kilimo kuhusu kukamilisha mkakati wa wa Taifa mawasiliano ili wakulima na wananchi waweze kujua namna ya kudhibiti tatizo la sumukuvu kwenye mazao hususan mahindi na karanga” alisisitiza Uwepo wa mkakati wa mawasiliano utasaidia jamii na wadau kuwa na uelewa mzuri juu ya tatizo la sumukuvu ambalo linaathiri mazao ya Kilimo kwa kusababisha ukosefu wa soko la uhakika kwa mazao yaliyoathirika, na pia kuathiri afya za walaji endapo mazao yameathiriwa na sumukuvu.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa kudhibiti Sumukuvu (TANIPAC) Ndugu Clepin Josephat alisema lengo la mradi huu ni kuhakikisha nchi inakuwa na usalama wa chakula na afya za walaji zinalindwa kwa mazao kutochafuliwa na sumukuvu. 

Clepin alipongeza jitihada za wadau waliowezesha kuandaliwa kwa rasimu ya mkakati wa mawasiliano ambao utasaidia kufikisha elimu kwa umma kwa njia rahisi na sahihi.

Takwimu zinazonyesha kuwa tangu kugundulika kwa tatizo la sumukuvu kwenye mazao mwaka 2016, watu 68 waliougua na kulazwa kutokana na kula chakula kilichochafuliwa na sumukuvu kwenye wilaya za Kiteto na Chemba ambapo watu 20 walifariki dunia.

“ Jumla ya watu 20 walipoteza maisha mwaka 2016 kwenye wilaya za Kiteto na Chemba kutokana na kula chakula kilichochafuliwa na sumukuvu,hivyo tunahitaji mkakati wa kufikisha elimu ya udhibiti sumukuvu kwa umma “ alisema Clepin.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Zanzibar Ndugu Hamad Masoud alisema katika
mwaka huu wafanyabiashara wengi toka Zanzibar watafika Bara kwa ajili ya kununua mazao ya chakula
hivyo uwepo wa elimu ya sumukuvu ni muhimu katika kuwalinda walaji.

Mradi wa kudhibiti sumukuvu unatekelezwa na Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano na Wizara za kisekta za
Afya,Mifugo,Viwanda na Biashara pamoja na sekta binafsi.

No comments:

Post a Comment

Pages