Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakijadiliana kwa pamoja
mambo yanayohusu mafunzo hayo.
Washiriki
wa Mafunzo
ya Mafunzo ya Haki za Binadamu , unyanyasaji na ukatili wa kijinsia
hususan kwa wanawake na watoto (wa kwanza kulia) ni Jaji wa Mahakama
ya
Rufani Tanzania, Mhe.Rehema Kerefu na (wa pili kulia) ni Jaji wa
Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Gerald
Ndika wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.(wa
tatu
kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake
Tanzania (TAWJA) ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Joaquine De
Mello.
Na Tawani Salum – Mahakama
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Jaji Gerald Ndika
amewataka Majaji na Mahakimu kutafsiri sheria zinaohusu masuala ya wanawake na
watoto ili ziendane na mazingira ya sasa katika kuendesha mashauri yanayohusu masuala
la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.
Akizunguza wakati wa Mafunzo ya Haki za Binadamu na Unyanyasaji hususani
kwa wanawake na watoto, yanayofanyika
Mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani Jaji Ndika alisema kuwa sheria zilizopo kwa kiwago kikubwa
zinajitosheleza kinachotakiwa jinsi ya kuzitafasiri, hivyo Majaji na Mahakimu watoe tafsiri ambayo
inaendana na mazingira ya matukio yalivyo.
Jaji Ndika
ambaye ni mshiriki katika mafunzo hayo,
alisema kuwa moja ya faida zake ni kuwaandaa wawezeshaji katika eneo
hilo ili kusaidia Mahakama ya Tanzania, Majaji wa Mahakama ya Rufani,Majaji wa
Mahakama Kuu, Mahakimu,watumishi mbalimbali ambao wanatoa maamuzi juu ya vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa wanawake
na watoto kuwa na umahiri.
‘‘Matukio haya yanatokana na mambo mengi ikiwemo mila potofu pamoja na uelewa wao mdogo, wanaona kumpiga mke au mtoto
ni jambo la kawaida na ana haki ya kufanya hivyo. Lakini ubora wa mafunzo haya
yatasaidia kupata wakufunzi ambao wataenda kuwapa wengine elimu juu ya kuweza
kupambana na ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto,’’ alisisitiza Jaji
Ndika. mafunzo hayo, alisema ni ya mara
ya tatu kufanyika yakiwa ni endelevu
katika kutoa elimu hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)
ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Joaquine De Mello akifungua rasmi mafunzo hayo, alisema kuwa yana lengo
la kuwawezesha watoa maamuzi kuwa na
uweledi zaidi wa kutoa haki na pia kuielimisha jamii juu ya haki zao za msingi na tatizo la unyanyasaji
na ukatili wa kijinsia ambalo limekithiri.
Aliongeza kwamba kumekuwa taarifa nyingi zinazotolewa na vyombo vya habari
pamoja na wanajamii ambao wamejitokeza wazi kutoa matukio mbalimbali juu ya
suala hilo. Pia tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa hivyo wamegundua kuwa
matukio mengi ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia yanafanywa wahusika wanaotuhumiwa kuwa ni familia au ndugu wa karibu.
Alisema kuna mapungufu katika jamii kama vile utamaduni wa kutokuwa na
utayari wa kusimamia na kuyapigia kelele tatizo hilo, ikiwa ni sababu mojawapo ya unyanyasaji na ukatili huo.
‘‘Kupitia mafunzo haya kama watoa maamuzi tunataka wapate jicho la
kipekee shauri linapokuja mbele yako mara moja unapata picha kuwa hili ni la
kikatili na unalipa nafasi yake na hii itasaidia katika kuandaa taarifa ya
matukio haya kwa usahihi, ikiwemo kuna takwimu ambazo tunazihitaji ili kujua
nguiu gani ya ziada inahitajika katika kusimamia jambo hili,’’ alisema Jaji De Mello.
Mshiriki mwingine wa mafunzo hayo, ambaye Hakimu Mkazi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Sokoine,iliyopo Jijini Dar es Salaam Mhe, Hanifa Mwingira alisema jamii inapaswa kuona
kuwa vitendo hivyo ni vibaya na kila mtu anapaswa kusema ‘ukatili sasa basi na
mtoto wa mwenzako kuwa ni mtoto wako na hupaswi kumfanyia ukatili,’.
Mwingira alifafanua kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi wa dini
ambao watawaelimisha waumini wao, wakiwemo Wenyeviti wa vijiji, kata pamoja na mitaa na
Maafisa wa Ustawi wa Jamii, Polisi, Magereza na wadau wengine wa sharia.
Mafunzo hayo yanayoendelea Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani yalihudhuriwa na
Majaji Wataafu kama vile Mh. Jaji Salum Massati ambaye anashiriki kama mtoa
mada.
Jumla ya washiriki 26 wanapatiwa mafunzo juu ya masuala ya unyanyasaji na ukatili kijinsi. Mafunzo hayo yameanza Juni 27, mwaka huu na yatamalizika
Julai Mosi, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment