Baadhi ya wana CCM waliojitokeza kujaza fomu za
kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa kugombea
tena nafasi ya urais katika uchaguzi ujao. Waziri Mkuu na Mbunge wa
Ruangwa, Kassim Majaliwa aliongoza zoezi hilo kwenye Ofisi ya CCM ya
wilaya hiyo, Juni 21,2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Baadhi ya wana CCM waliojitokeza kujaza fomu za
kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa kugombea
tena nafasi ya urais katika uchaguzi ujao. Waziri Mkuu na Mbunge wa
Ruangwa, Kassim Majaliwa aliongoza zoezi hilo kwenye Ofisi ya CCM ya
wilaya hiyo, Juni 21,2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati mwanachama wa CCM,
Jacob Masumbuko alipotia saini fomu ya kumdhamini, Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ili aweze kuteuliwa kuteuliwa tena kugombea urais. Zoezi hilo
lilifanyika kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya ya Rungwa, Juni 21, 2020.
Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa LIndi, Fadhili Juma.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Makuu,
Kasim Majaliwa akishuhudia wakati wana CCM walipojitokeza kujaza fomu
za kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa tena
kugombea urais katika uchaguzi ujao. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM
wa mkoa wa Lindi , Fadhili Juma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Makuu, Kasim Majaliwa akishuhudia wakati wana CCM walipojitokeza
kujaza fomu za kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze
kuteuliwa tena kugombea urais katika uchaguzi ujao. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi , Fadhili Juma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi fomu zenye majina , saini za wana CCM waliomdhamini Rais Dkt.
John Magufuli ili aweze kugombea tena urais Mwenyekiti wa CCM wa wilaya
ya Ruangwa, Said Kaondo baada ya kumaliza zoezi la udhamini kwenye
Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Juni 21, 2020.Katikati ni Mwenyekiti
wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Fadhili Juma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akigonganisha kiwiko na Mwenyekiti wa CCM wa
wilaya ya Ruangwa, Said Kaondo baada ya kumkabidhi fomu zenye majina na
saini za wana CCM waliomdhamini Rais Dkt.
John Magufuli ili aweze kugombea tena urais. Tukio hilo lilifanyika
kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Juni 21, 2020. Katikati ni
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Fadhili Juma. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza wanachama 314 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wilayani Ruangwa, Lindi katika kujaza fomu za kumdhamini Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ili aweze kuteuliwa kugombea tena nafasi ya urais.
Idadi
hiyo inafanya jumla ya wanachama waliojitokeza kumdhamini Rais Dkt. Magufuli
katika wilaya hiyo kufikia 2,565 baada ya wanachama wengine 2,251 kujaza fomu
hizo jana (Jumamosi, Juni 20, 2020) na kumdhamini kiongozi huyo.
Waziri
Mkuu ameongoza wanachama hao wa CCM leo (Jumapili, Juni 21, 2020) katika ofisi
za CCM wilayani Ruangwa. Amewasihi wananchi hao waendelee kuwa na imani na Rais
Dkt. Magufuli pamoja na Serikali anayoiongoza.
“Mheshimiwa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi zote alizoziahidi ikiwemo ya
kuwatumikia Watanzania wote hasa wanyonge. Amewatumikia Watanzania wote bila ya
kujali itikadi zao za kisiasa na hata za kidini. Nawapongeza wana CCM wenzangu
mliojitokeza kumdhamini rais wetu.”
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa “Kitendo mlichokifanya leo kinaonyesha shukrani kubwa kwa
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye wakati wote ameonesha mapenzi
makubwa kwetu pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.”
Amesema kwa
sasa wilaya ya Ruangwa imepata mabadiliko makubwa kimaendeleo ambayo hapo awali
hayakuwepo kama nishati ya umeme, maji ambayo kwa sasa kila kijiji kina kisima,
shule za msingi katika kila kijiji na sekondari kwenye kata zote pamoja na
barabara za lami katika mitaa ya mji wa Ruangwa.” Haya yote ni Dkt. Mgufuli.”
Kwa uapande wake,
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi, Fadhili Juma amesema wanaCCM wa mkoa huo wapo
bega kwa bega na Rais Dkt. Magufuli na kwamba watahakikisha anapata kura nyingi
katika uchaguzi ujao.
Awali, Waziri Mkuu aliwashukuru
WanaRuangwa wote kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha miaka
mitano ambao ulimuwezesha kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea maendeleo kwa
ufanisi mkubwa.
No comments:
Post a Comment