HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 28, 2020

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHITIMISHA ZIARA YA KICHAMA MKOA WA DSM

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya Mkoa wa Dar es Salaam alipowasili katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam leo Juni 27,2020 kwa ajili ya mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya Kichama katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo  na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Zakaria Mwasasu  wakati wa mkutano wa Majumuisho ya ziara yake ya Kichama Mkoa wa Dar es Salaam kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Dar es Salaam  leo Juni 27,2020 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Ilala Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salam.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa Majumuisho ya ziara yake ya Kichama ya Mkoa wa Dar es Salaam leo Juni 27,2020 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Ilala Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salam.

No comments:

Post a Comment

Pages