HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2020

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE KUAPISHWA RAIS MPYA WA BURUNDI

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura Nchini Burundi kwa ajili ya kumuwaklilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye shughuli ya kuapishwa Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye  leo Juni 18,2020. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Gasten Sindimwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais  Mpya wa  Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi  alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye leo Juni 18,2020. kushoto ni Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Gasten Sindimwo alipowasili  kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bujumbura Nchini Burundi kwa ajili ya kumuwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye shughuli ya kuapishwa Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye  leo Juni 18,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 
Rais  Mpya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye  akikaguwa Gwaride baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Nchini Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa  na Rais mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakati Rais Ndayishimiye alipokuwa akipokea Gwaride la Jeshi la Wananchi wa Burundi baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Igoma Stadium Nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shughuli hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais  Mpya wa  Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi  alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye leo Juni 18,2020. kushoto ni Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete  wakiwa katika picha ya pamoja na  Rais  Mpya  wa Burundi Mhe.  Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega nchini Burundi leo Juni 18,2020. 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alikuwa miongoni mwa Viongozi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Burundi  Evariste Ndayishimiye zilizofanyika jana katika Mji wa Gitega, Uwanja wa  Igoma Stadium Nchini Burundi.
Katika sherehe hizo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Akitoa salam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. samia Suluhu Hassan , amempongeza Rais Ndayishimiye kwa ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa hivi karibuni na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Burundi katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Makamu wa Rais Mhe. samia pia aliwapa pole Wananchi wa Burundi kwa kwa msiba mkubwa wa aliyekuwa Rais wa Nchi yao marehemu Pierre Nkurunziza na kuwataka wawe na subira katika kipindi kiki cha maombolezo.
Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiambatana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na NaibuWaziri wa Mambo ya Nje Dkt.   walipata nafasi ya kufika  nyumbani kwa marehemu Nkurunziza  Jijini Bujumbura kwa ajili ya kuitembelea na kuifariji familia akiwemo mjane na watoto wa marehemu, ambapo amemuomba Mwenyezi Mungu kuwapa uvumilivu na kuwa na subira katika kipindi hiki cha maombolezo.
Katika sherehe hizo za kuapishwa Rais mpya wa Burundi pia zilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amerejea Nchini akitokea Nchini Burundi jana Usiku.

No comments:

Post a Comment

Pages