HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2020

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA UBUNGO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Ubungo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili wakati akitokea Mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James kuhusu changamoto ya Usafiri wa Bajaji aliyokuwa akiomba kupewa ili imsaidie kuendesha familia yake.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Nyangoma James Mama mwenye Ulemavu wa miguu msaada wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kununulia Bajaji ili imsaidie kuendesha Maisha yake. Pia Rais Dkt. Magufuli aliendesha Mchango kwa Wananchi wengine ambapo waliahidi kumchangia mama huyo kiasi cha Shilingi Milioni 3.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5. kushoto aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makore.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa Bajaji.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akicheza Wimbo wa hamasa pamoja na Wananchi wa Ubungo mara baada ya kuwahutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la Ubungo Darajani mara baada ya kuzungumza na Wananchi. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la Ubungo Darajani mara baada ya kuzungumza na Wananchi. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages