HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 08, 2020

Mkwasa aizodoa Bodi ya Ligi Kuu

Na Mwandishi Wetu

KOCHA Msaidizi wa klabu ya Yanga Boniface Mkwasa ameizodoa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB)  kwa jinsi ambavyo imepanga ratiba pasipo kujali hali ya kiuchumi ya klabu za Ligi Kuu wakati huu ambapo michezo inarejea.

Mkwasa amefikia hatua hiyo kutokana na ratiba inayokikabili kikosi chake katika mitanange ya VPL Ligi inapoenda kurejea kuanzia juni 13 wikiendi ijayo.

Yanga inakabiliwa na michezo 11 ya Ligi Kuu Tanzania Bara kumaliza msimu huu wa 2019/20 jambo ambalo litawafanya kucheza michezo yote kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

"Tuna ratiba ngumu sana nadhani Bodi ya Ligi ilipaswa kulitazama hilo,  tukiwa wakweli klabu haziko imara kiuchumi hivyo ratiba ilipaswa kuwa rafiki japo sio rahisi.

"Kwa mfano tunaanzia Shinyanga kisha tunarudi Dodoma alafu twende Kagera!!  unajiuliza kwa nini tukitoka Shinyanga tusiende Kagera afu ndio tuje Dodoma!? "alisema

"Nadhani hili wanapaswa kulitazama upya kwa sababu jiografia ya nchi yetu ni kubwa mno hivyo ni bora timu inapoenda ukanda mmoja ikamaliza kabisa michezo yake na klabu za kanda hiyo.

"Lakini pia hizo gharama zitakuwa juu ya nani maana hali ya kiuchumi kwa klabu zetu ni wazi ni ngumu, lakini pia hao wachezaji usalama wao tunauweka wapi kutoka mchezo mmoja hadi mwingine na muda wa kusafiri?! "alisema Mkwasa.

Aliongeza kuwa TPLB wananafsi ya kulitazama hilo upya ili kuzisaidia klabu Pamoja na kuangalia afya za wachezaji wakati huu ambao wanarejea dimbani baada ya kukaa kwa muda mrefu pasipo ushindani.

Yanga iko nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL wakiwa na pointi 51 michezo 27 nyuma ya Azam FC nafasi ya pili pointi 54 michezo 28 huko Simba SC wakitakata kileleni na pointi zao 71 michezo 28.

Ili Yanga kupambania ubingwa itawalazimu kushinda michezo yao yote 11 Iliyosalia huko wakimuombea njaa Mnyama wa Mwitu Simba SC kupoteza michezo sita kati ya 10 aliyonayo mkononi.

No comments:

Post a Comment

Pages